Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Mageuzi Ni Jambo Hakika?
    Amkeni!—2006 | Septemba
    • Kijitabu kilichochapishwa mnamo 1999 na Shirika la Kitaifa la Sayansi (NAS) nchini Marekani kilisema hivi: “Mfano mmoja wenye kusadikisha wa mageuzi ya spishi mpya ulihusisha spishi 13 za shorewanda waliochunguzwa na Darwin katika Visiwa vya Galápagos. Ndege hao sasa wanaitwa shorewanda wa Darwin.”

      Katika miaka ya 1970, watafiti kadhaa wakiongozwa na Peter na Rosemary Grant, walianza kuwachunguza shorewanda hao na wakagundua kwamba baada ya mwaka mzima wa ukame, idadi ya shorewanda wenye midomo mirefu waliosalimika ilizidi ile ya wale wenye midomo mifupi. Kwa kuwa ukubwa na umbo la midomo yao ndiyo njia moja kuu ya kutambulisha spishi hizo 13 za shorewanda, huo ulidhaniwa kuwa ugunduzi muhimu. Kijitabu hicho cha NAS kinasema, “Peter na Rosemary Grant wamekadiria kwamba ikiwa visiwa hivyo vitakumbwa na ukame mwaka moja katika kila kipindi cha miaka 10, spishi mpya ya shorewanda itatokezwa baada ya miaka 200 hivi.”

      Hata hivyo, kile kijitabu cha NAS hakizungumzii baadhi ya mambo hakika yenye kuaibisha. Katika miaka iliyofuata mwaka huo wa ukame, shorewanda wenye midomo mifupi walikuwa wengi tena kuliko wale wenye midomo mirefu. Hivyo mnamo 1987, Peter Grant na mhitimu wa chuo kikuu, Lisle Gibbs, waliandika katika jarida la sayansi Nature kwamba walishuhudia “uteuzi ukichukua mkondo ulio kinyume.” Katika 1991, Grant aliandika kwamba “idadi ya ndege, ikiongozwa na uteuzi wa kiasili, ilikuwa ikiongezeka na kupungua,” kila mara hali ya hewa ilipobadilika. Watafiti hao waligundua pia kwamba ndege wa “spishi” kadhaa tofauti walizalisha pamoja na kutokeza ndege waliostahimili kuliko wazazi wao. Peter na Rosemary Grant walikata kauli kwamba ikiwa ndege hao wangeendelea kuzalisha pamoja, baada ya kipindi cha miaka 200 hivi, “spishi” hizo mbili zingeungana na kuwa spishi moja.

  • Je, Mageuzi Ni Jambo Hakika?
    Amkeni!—2006 | Septemba
    • Kwa kweli, shorewanda wa Darwin hawabadiliki na “kuwa ndege wapya.” Bado wao ni shorewanda. Na uhakika wa kwamba wanazalisha pamoja unatilia shaka mbinu za wanasayansi fulani za kuainisha spishi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki