Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Babuloni Mkubwa Ameanguka!”
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • “Na yeye atateswa kwa moto na salfa katika mwono wa malaika watakatifu na katika mwono wa Mwana-Kondoo.

  • “Babuloni Mkubwa Ameanguka!”
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Ufunuo 14:10b,

  • “Babuloni Mkubwa Ameanguka!”
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 15, 16. Ni nini maana ya maneno “moto na salfa” kwenye Ufunuo 14:10?

      15 Baadhi ya watu wameona mtajo hapa wa “moto na salfa” (“moto na kiberiti,” Union Version) kuwa ushuhuda wa kuwako kwa mahali pa moto wa mateso. Lakini mtazamo mfupi wa unabii unaofanana na huu huonyesha maana halisi ya maneno hayo katika muktadha huu. Huko nyuma katika siku za Isaya, Yehova alionya taifa la Edomu kwamba wao wangeadhibiwa kwa sababu ya uadui wao kuelekea Israeli. Yeye alisema: “Vijito vyake vitageuzwa kuwa lami, na mavumbi yake yatageuzwa kuwa kiberiti [salfa, NW] na ardhi yake itakuwa lami iwakayo. Haitazimwa mchana na usiku, moshi wake utapaa milele. Tangu kizazi hata kizazi itakuwa ukiwa; hapana mtu atakayepita kati yake milele na milele.”—Isaya 34:9, 10.

      16 Je! Edomu ilivurumishwa ndani ya mahali pa kifumbo penye moto ichomeke milele? Bila shaka sivyo. Badala ya hivyo, taifa hilo lilitoweka kabisa kutoka mandhari ya ulimwengu kana kwamba lilikuwa limeliwa kabisa na moto na salfa. Tokeo la mwisho la adhabu hiyo halikuwa mateso ya milele bali “utupu . . . ukiwa . . . si kitu.” (Isaya 34:11, 12) ‘Kupaa milele kwa moshi’ hutoa kielezi cha hili waziwazi. Nyumba inapoteketea, moshi huendelea kutoka katika majivu kwa wakati fulani baada ya miale kufa, ukiandalia watazamaji ithibati ya kwamba kulikuwako mteketezo wenye kuharibu. Hata leo watu wa Mungu hukumbuka somo wanaloweza kujifunza kutokana na uharibifu wa Edomu. Kwa njia hiyo ‘moshi wa kuchomeka kwayo’ ungali unapaa kwa njia ya ufananisho.

      17, 18. (a) Ni nini tokeo kwa wale ambao hupokea alama ya hayawani-mwitu? (b) Ni katika njia gani waabudu wa hayawani-mwitu huteswa? (c) Ni jinsi gani “moshi wa kuteswa kwao hupaa milele na milele”?

      17 Wale walio na alama ya hayawani-mwitu wataharibiwa kabisa pia, kana kwamba kwa moto. Kama unabii unavyofunua baadaye, miili yao mifu itaachwa bila kuzikwa iliwe na wanyama na ndege. (Ufunuo 19:17, 18) Kwa wazi, basi, wao hawateswi milele! Wao ‘huteswaje kwa moto na salfa’? Kwa njia ya kwamba mbiu ya ukweli huwafichua na kuwaonya juu ya hukumu ya Mungu inayokuja. Kwa hiyo wao wanasuta watu wa Mungu na, inapowezekana wanashawishi kwa uayari hayawani-mwitu wa kisiasa anyanyase na hata kuua Mashahidi wa Yehova.

  • “Babuloni Mkubwa Ameanguka!”
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 18 Ni nani leo wanaopeleka ujumbe wenye kutesa? Kumbuka, wale nzige wa ufananisho wana mamlaka ya kutesa watu ambao hawana muhuri wa Mungu juu ya vipaji vya nyuso zao. (Ufunuo 9:5) Kwa wazi, hawa wakiwa chini ya mwelekezo wa kimalaika ndio ‘watesaji.’

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki