Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kwa Nini Ushirikiano Ni Muhimu?
    Amkeni!—2005 | Septemba 8
    • Kwa kuwa viboko hukaa majini kwa muda mrefu, wao husafishwa na “rafiki” zao wenye manyoya na mapezi. Kiboko anapokuwa majini, samaki anayeitwa black labeo, ambaye ni jamii ya kambare, husafisha mwani, ngozi iliyokufa, wadudu, au kitu chochote kinachokwama juu ya mnyama huyo. Hata wao husafisha meno na fizi za viboko! Jamii nyingine za samaki pia husaidia kwa kusafisha vidonda na nyingine hutumia pua zao ndefu kupenya na kula katikati ya vidole vya miguu vya kiboko na sehemu nyingine zisizofikika kwa urahisi.

      Bila shaka, samaki ni mwenye kuvutia, hivyo anahitaji kuondolewa uchafu unaokwama juu yake, kama vile wanyama wenye magamba na bakteria, kuvu, na viroboto, na vilevile tishu zilizoharibika au zenye ugonjwa. Ili kusafishwa, kwa kawaida samaki wa baharini huenda mahali pa kusafishiwa. Wanapofika huko, goby wenye rangi nyangavu, laburida, na uduvi huwasafisha samaki hao vizuri kabisa, na palepale wanapata chakula. Huenda samaki wakubwa wakasafishwa na kikundi kikubwa cha viumbe hao!

      Samaki anayetaka kusafishwa anaweza kuonyesha hivyo kwa njia nyingi. Kwa mfano, wengine husimama kwa njia isiyo ya kawaida wakiweka kichwa chini na mkia juu. Au huenda wakafungua kinywa na mashavu yao, kana kwamba wanasema: “Ingieni tu. Sitawauma.” Viumbe hao wanaosafisha hukubali bila wasiwasi, hata ikiwa mteja wao ni hatari, kama vile kungamorei au papa. Wanaposafishwa, wateja fulani hubadili rangi, labda ili kufanya wadudu waonekane kwa urahisi zaidi. Katika maji yasiyo na samaki ambao huwasafisha wengine, samaki wa baharini “huathiriwa na wadudu haraka na kuwa wagonjwa,” kinasema kitabu Animal Partnerships. “Lakini mara tu samaki ambaye husafisha anapoingizwa katika maji hayo, yeye huanza kufanya kazi ya kuwasafisha na ni kana kwamba wao hujua ni nini kinachoendelea kwani wao hupanga foleni mara moja ili wasafishwe.”

  • Kwa Nini Ushirikiano Ni Muhimu?
    Amkeni!—2005 | Septemba 8
    • [Picha katika ukurasa wa 10]

      Uduvi msafishaji mwenye madoa-doa akiwa juu ya “anemone”

      [Picha katika ukurasa wa 10]

      Samaki anayeitwa “butterfly” akiwa pamoja na samaki mdogo msafishaji

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki