-
Maisha Katika Nyakati za Biblia MvuviMnara wa Mlinzi—2012 | Agosti 1
-
-
“Wakakusanya Samaki Wengi Sana”
Leo, kama ilivyokuwa katika karne ya kwanza, maeneo yenye samaki wengi katika Bahari ya Galilaya yako karibu na milango ya vijito na mito inayoleta maji katika bahari hiyo. Katika maeneo hayo, mimea huingia baharini na kuwavutia samaki.
-
-
Maisha Katika Nyakati za Biblia MvuviMnara wa Mlinzi—2012 | Agosti 1
-
-
Kisha, wanaume waliokuwa kando ya bahari walikokota wavu ili kuwaleta samaki ufuoni na kuwachagua. Waliwaweka samaki wazuri ndani ya mitungi. Wengine wao waliuzwa katika eneo hilo kabla hawajakaushwa. Wengi wao walikaushwa na kutiwa chumvi au siki, kisha wakahifadhiwa ndani ya mitungi iliyotengenezwa kwa udongo na kusafirishwa hadi Yerusalemu au nchi nyinginezo. Viumbe wasio na magamba na mapezi, kama vile mikunga, walionwa kuwa wasio safi na walitupwa. (Mambo ya Walawi 11:9-12)
-
-
Maisha Katika Nyakati za Biblia MvuviMnara wa Mlinzi—2012 | Agosti 1
-
-
Kati ya samaki waliotafutwa na wavuvi wa karne ya kwanza ni samaki wanaopatikana kwa wingi wanaoitwa tilapia. Samaki hao waliliwa kwa ukawaida na watu wengi huko Galilaya, na inaelekea Yesu alikula samaki hao wenye ladha tamu. Huenda alitumia tilapia waliokaushwa na kutiwa chumvi alipofanya muujiza wa kulisha maelfu ya watu kwa kutumia samaki wawili. (Mathayo 14:16, 17; Luka 24:41-43) Mara nyingi samaki hao huogelea wakiwa wamebeba samaki wadogo kinywani. Hata hivyo, ikiwa hawabebi samaki wadogo, yaelekea wanabeba jiwe dogo, au huenda wakaokota sarafu inayong’aa iliyolala chini ya bahari.—Mathayo 17:27.
-