-
Kusafiri kwa Mashua Huko KeralaAmkeni!—2008 | Aprili
-
-
Kuvua Katika Eneo Hilo
Uvuvi ni sehemu ya maisha katika eneo hilo. Jambo moja ambalo huenda huwezi kamwe kujionea mahali pengine popote ni wanawake wakivua samaki wanaoitwa karimeen kwa mikono. Samaki hao wanaopatikana tu huko Kerala, wanapendwa sana na Wahindi na wageni. Wanapotafuta samaki hao, wanawake hutembea kwa miguu ndani ya maji huku sufuria zao zikielea nyuma yao. Samaki wanapowaona wanawake hao wakikaribia, wanapiga mbizi na kuficha vichwa vyao kwenye matope. Ili samaki wasiwashinde akili, wanawake hao hupapasa-papasa kwenye matope hayo kwa miguu yao ambayo imezoea kazi hiyo na kuwapata. Kisha, wanatumbukiza mikono yao upesi ndani ya maji na kuwashika samaki hao wasiotazamia kisha wanawaingiza ndani ya sufuria. Wakiisha kushika samaki wa kutosha, wanarudi ufuoni ambako wanunuzi wanawasubiri kwa hamu. Samaki wakubwa zaidi na wanaouzwa kwa bei ya juu zaidi wananunuliwa na hoteli za kifahari ambako matajiri wanafurahia kuwala, huku samaki wadogo wakiwa mlo mtamu kwa ajili ya watu wenye mapato ya chini.
-
-
Kusafiri kwa Mashua Huko KeralaAmkeni!—2008 | Aprili
-
-
[Picha katika ukurasa wa 23]
Wanawake wakivua samaki kwa mikono
-