Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Vitu vya Kuchukiwa na Mataifa Yote”
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Baada ya Mashahidi kama 1,200 kufungwa katika Ujerumani mapema katika enzi ya Nazi kwa kukataa kutoa salamu ya Nazi na kukataa kuvunja kutokuwamo kwao kwa Kikristo, maelfu walitendwa vibaya kimwili katika Marekani kwa sababu walikataa kusalimu bendera ya Amerika. Wakati wa juma la Novemba 4, 1935, idadi fulani ya watoto wa shule katika Can­ons­burg, Pennsylvania, walipelekwa kwenye chumba cha kuchemshia maji na kuchapwa viboko kwa kukataa kusalimu bendera. Grace Es­tep, aliyekuwa mwalimu, aliachishwa wadhifa wake katika shule hiyo kwa sababu iyo hiyo. Mnamo Novemba 6, William na Lillian Gobitas walikataa kusalimu bendera na wakafukuzwa shuleni katika Minersville, Pennsylvania. Baba yao alipeleka mashtaka mahakamani ili watoto wake waruhusiwe kwenda shuleni. Mahakama ya wilaya ya jimbo na mahakama ya mzunguko ya rufani pia ziliamua kesi kwa kuwapendelea Mashahidi wa Yehova. Hata hivyo, katika 1940, huku taifa likikaribia kuingia vitani, Mahakama Kuu ya Marekani, katika Minersville ­School District v. Gobitis, iliunga mkono sharti la kusalimu bendera kwa shule zote za umma, kwa uamuzi wa 8 kwa 1. Hiyo iliongoza kwenye jeuri ya taifa lote dhidi ya Mashahidi wa Yehova.

      Kulikuwa na mashambulizi mengi sana ya jeuri dhidi ya Mashahidi wa Yehova hivi kwamba Bi. Eleanor Roosevelt (mke wa Rais F. D. Roosevelt) ­alisihi umma uache jeuri hiyo. Mnamo Juni 16, 1940, msaidizi wa wakili mkuu wa Marekani, Francis Biddle, katika matangazo ya redio ya kutoka pwani moja hadi ile nyingine, alirejezea kihususa maovu waliyotendwa Mashahidi na akasema kwamba hayo hayangevumiliwa. Lakini hilo halikukomesha maovu hayo.

      Katika kila hali inayoweza kuwaziwa—barabarani, mahali pa kazi, Mashahidi walipozuru nyumba katika huduma yao—bendera ziliwekwa mbele yao, kwa dai kwamba wazisalimu—au sivyo wangekiona! Mwishoni mwa 1940, Kitabu-Mwaka cha Mashahidi wa Yehova kiliripoti: “Viongozi wa kidini na Jeshi la Amerika, kupitia magenge kama hayo yanayotenda bila kujali sheria, walileta uharibifu mkubwa wa jeuri. Mashahidi wa Yehova wametendwa vibaya, wakapigwa, wakatekwa nyara, wakafukuzwa katika miji, wilaya na majimbo, wakamwagiwa lami na manyoya, wakalazimishwa kunywa mafuta ya mbarika, wakafungwa pamoja na kukimbizwa barabarani kama hayawani wapumbavu, wakahasiwa na kulemazwa, wakaudhiwa na kutukanwa na umati wa kiibilisi, wakafungwa kwa mamia bila mashtaka na kufungwa bila njia ya kuwasiliana na wengine na kunyimwa pendeleo la kuwasiliana na watu wa ukoo, marafiki au mawakili. Mamia yao wengine wamefungwa gerezani na kuwekwa katika kile kiitwacho eti ‘kifungo cha ulinzi’; wengine wamepigwa risasi usiku; wengine wakatishwa kunyongwa na kupigwa hadi wakazimia. Namna mbalimbali ya jeuri ya magenge imetukia. Wengi wameraruliwa nguo zao, Biblia zao na fasihi nyinginezo zikatwaliwa na kuchomwa hadharani; magari yao, nyumba za trela, makao yao na sehemu za kusanyiko zikaharibiwa na kuchomwa . . . Katika visa vingi ambavyo kesi zimefanywa katika jumuiya zinazoongozwa na magenge, mawakili pamoja na mashahidi wamezingirwa na umati na kupigwa wanapoenda mahakamani. Katika karibu kila kisa ambako kumekuwa na jeuri ya magenge maofisa wa umma hawakufanya lolote na walikataa kutoa ulinzi, na katika visa kadhaa polisi wameshiriki katika magenge hayo na nyakati nyingine hata kuongoza magenge hasa.” Kuanzia 1940 hadi 1944, magenge zaidi ya 2,500 yenye jeuri yaliwadhulumu Mashahidi wa Yehova katika Marekani.

      Kwa sababu watoto wengi wa Mashahidi wa Yehova walifukuzwa shuleni, kwa muda fulani wakati wa miaka ya mwishoni mwa 1930 na mapema miaka ya 1940 ilihitajika kwamba wao waendeshe shule zao wenyewe katika Marekani na Kanada ili kuandaa elimu kwa watoto wao. Hizo ziliitwa Shule za Ufalme.

  • “Vitu vya Kuchukiwa na Mataifa Yote”
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Si kila mtu amekubaliana na hatua hizo za uonevu dhidi ya watu ambao, kwa sababu ya dhamiri, hujizuia kwa staha kushiriki katika sherehe za uzalendo. The Open Forum, kilichochapishwa na Tawi la California Kusini la Shirika la Haki za Umma la Marekani, kilisema hivi katika 1941: “Wakati umefika wa sisi kutumia akili kuhusu jambo hili la kusalimu bendera. Mashahidi wa Yehova si Waamerika wasio waaminifu. . . . Wao si wavunja sheria kwa ujumla, bali huishi maisha yanayofaa, na yenye utaratibu, wakishiriki sehemu yao katika mambo yanayowafaa wote.” Katika 1976 mwandikaji safu za magazeti katika Argentina, katika Herald ya Buenos Aires, alionelea waziwazi kwamba “itikadi [za Mashahidi] ni zenye kuudhi kwa wale tu wanaofikiria kuwa uzalendo ni jambo hasa la kupeperusha bendera na kuimba wimbo wa taifa, na si jambo la moyoni.” Yeye aliongeza: “Hitler na Stalin waliwaona [Mashahidi] kuwa wasiovumilika, na kuwatenda vibaya sana. Madikteta wengine wengi wakitamani kuwafanya waridhiane wamejaribu kuwakandamiza. Na wameshindwa.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki