-
Ni Maridadi na Matamu!Amkeni!—2004 | Desemba 8
-
-
Mung’unye
Kuna maandishi ya karne ya 16 yanayoonyesha kwamba ua la mung’unye (Cucurbita pepo) lililiwa katika mabara ya Amerika, na inaonekana kwamba wenyeji wa asili wa Amerika walikula tu maua ya kiume (yale yaliyokuwa na mashina marefu na membamba) ili kuyaacha maua ya kike (yale yenye tunda dogo sana) yazalishe. Kabla ya kuyapika maua hayo, ondoa majani ya nje yenye miiba. Unaweza kutoa au kuacha sehemu ya kike inayotoa mbegu. Unaweza kufurahia utamu wa maua ya mung’unye ukitayarisha milo na mchuzi kwa mafuta ya mzeituni, mahindi mabichi, na tunda la mung’unye. Ili ladha hiyo ikolee zaidi, kaanga maua ya mung’unye kwa kitunguu, kitunguu-saumu, na viungo vingine unavyopenda. Au unaweza pia kutia mchanganyiko wa jibini, vitunguu, na viungo ndani ya maua hayo. Ukiisha kufanya hivyo, funga miisho yake na uyachovye ndani ya sehemu nyeupe za mayai yaliyopigwa-pigwa na kuchanganywa na viini vya mayai. Mwishowe, nyunyiza chengachenga za mkate juu ya maua hayo halafu uyakaange, nawe utafurahia utamu wake wa pekee!
-
-
Ni Maridadi na Matamu!Amkeni!—2004 | Desemba 8
-
-
[Picha katika ukurasa wa 23]
Ua la mung’unye
-