-
Njia ya 1—Kula VizuriAmkeni!—2011 | Machi
-
-
Njia ya 1—Kula Vizuri
“Kula chakula. Usile kingi. Kula hasa mboga.” Kwa maneno hayo machache, mwandishi Michael Pollan anaeleza kwa ufupi mazoea ya kula yanayofaa ambayo yametumiwa kwa muda mrefu. Anamaanisha nini?
◯ Kula vyakula ambavyo havijatengenezwa viwandani. Kula vyakula “halisi”—vyakula vinavyotolewa moja kwa moja kutoka shambani ambavyo watu wamekuwa wakila kwa miaka mingi—badala ya vyakula vya kisasa vilivyotengenezwa viwandani. Kwa kawaida, vyakula vilivyotengenezwa viwandani na vyakula vyepesi vya mikahawa vina sukari, chumvi, na mafuta mengi, na inadhaniwa kwamba vitu hivyo husababisha magonjwa ya moyo, kiharusi, kansa, na magonjwa mengine hatari. Unapopika, jaribu kuchemsha, kuoka, na kuchoma badala ya kukaanga chakula. Jaribu kutumia vikolezo na viungo ili usitumie chumvi nyingi. Hakikisha kwamba nyama imeiva vizuri, na usile kamwe chakula kilichoharibika.
-
-
Njia ya 1—Kula VizuriAmkeni!—2011 | Machi
-
-
◯ Kula hasa mboga. Chakula chenye lishe kinatia ndani matunda mbalimbali, mboga, na nafaka isiyokobolewa maganda badala ya nyama na vyakula vyenye wanga. Mara moja au mbili kwa juma, jaribu kula samaki badala ya nyama. Punguza vyakula vilivyotolewa virutubisho kama vile tambi, mkate mweupe, na mchele mweupe. Lakini epuka mazoea hatari ya kula yanayofuatwa na watu ili kupunguza uzito. Wazazi, lindeni afya ya watoto wenu kwa kuwasaidia wawe na mazoea ya kula vyakula vyenye lishe. Kwa mfano, wapeni kokwa na matunda na mboga zilizosafishwa vizuri badala ya viazi vilivyokaangwa au peremende.
-