Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kupambana na Hayawani Wawili Wakali Sana
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • “Na yeye huweka chini ya mshurutisho watu wote, wadogo na wakubwa, na matajiri na maskini, na walio huru na watumwa, kwamba imewapasa wao kuwapa hawa alama katika mkono wao wa kulia au juu ya kipaji cha uso wao,

  • Kupambana na Hayawani Wawili Wakali Sana
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Ufunuo 13:16

  • Kupambana na Hayawani Wawili Wakali Sana
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 35. Inamaanisha nini kutiwa alama ya jina la hayawani-mwitu juu ya kipaji cha uso au katika mkono wa kulia?

      35 Humaanisha nini kutiwa alama ya jina la hayawani-mwitu juu ya kipaji cha uso au katika mkono wa kulia? Wakati Yehova alipowapa Israeli Sheria, yeye aliwaambia: “Ni lazima nyinyi mtumie maneno yangu haya kwenye moyo wenu na nafsi zenu na kuyafunga hayo kama ishara juu ya mikono yenu, na hayo lazima yatumike kuwa ukanda wa pajini kati ya macho yenu.” (Kumbukumbu 11:18, NW) Hiyo ilimaanisha kwamba ilikuwa sharti Waisraeli waweke daima Sheria hiyo mbele yao, hivi kwamba ikavuta matendo na mawazo yao yote. Wapakwa-mafuta 144,000 wasemwa kuwa wana jina la Baba na la Yesu limeandikwa juu ya vipaji vya nyuso zao. Hilo huwatambulisha kuwa ni wa Yehova Mungu na Yesu Kristo. (Ufunuo 14:1) Katika kuiga, Shetani anatumia alama ya roho waovu ya hayawani-mwitu. Mtu yeyote anayeshughulika na utendaji wa kila siku kama vile kununua na kuuza hubanwa afanye kwa njia ambayo hayawani-mwitu hufanya, kama, mathalani, katika kusherehekea sikukuu. Wao wanatarajiwa kuabudu hayawani-mwitu, wakimruhusu atawale maisha zao, ili kupokea alama yake.

      36. Wale wanaokataa kukubali alama ya hayawani-mwitu wamekuwa na matatizo gani?

      36 Wale wanaokataa kukubali alama ya hayawani-mwitu wamekuwa na matatizo daima. Mathalani, kuanzia miaka ya 1930, wao walilazimika kupiga mapigano mengi ya mahakamani na kuvumilia kufanyiwa ghasia nyingi za kijeuri na minyanyaso mingine. Katika nchi za watawala wenye kudai utii wote, walitupwa ndani ya kambi za mateso, ambamo wengi walikufa. Tangu vita ya ulimwengu ya pili, vijana wasiohesabika wametaabishwa na vifungo virefu, baadhi yao hata wakateswa na kuuawa, kwa sababu ya kukataa kuacha msimamo wao wa kutokuwamo kwa Kikristo. Katika mabara mengine Wakristo hawawezi kununua au kuuza kihalisi; wengine hawawezi kumiliki mali; wengine wanalalwa kinguvu, wanauawa kimakusudi, au wanafukuzwa kutoka bara la uzawa wao. Kwa sababu gani? Kwa sababu katika dhamiri njema wao wanakataa kununua kadi ya chama cha kisiasa.d—Yohana 17:16.

      37, 38. (a) Ni kwa nini ulimwengu ni mahali penye magumu kwa wale wanaokataa kuwa na alama ya hayawani-mwitu? (b) Ni nani wanaoshika ukamilifu, nao wameazimia kufanya nini?

      37 Katika maeneo fulani ya dunia, dini imeimarika sana katika maisha ya watu wa jumuiya hivi kwamba yeyote anayechukua msimamo kwa ajili ya ukweli wa Biblia anatengwa mbali na jamaa na marafiki wa zamani. Inataka imani kubwa kuvumilia. (Mathayo 10:36-38; 17:22) Katika ulimwengu ambamo wengi huabudu ukwasi wa kimwili na ambao utovu wa haki unaenea pote, mara nyingi Mkristo wa kweli sharti aitibari Yehova kabisa kabisa kwamba Yeye atamtegemeza katika kufuatia mwendo wa unyofu. (Zaburi 11:7; Waebrania 13:18) Katika ulimwengu wenye kufurika ukosefu wa adili, inataka azimio kubwa ili kubaki safi na mwenye kutakata. Wakristo wanaokuwa wagonjwa mara nyingi hubanwa na madaktari na waaguzi wavunje sheria ya Mungu juu ya utakato wa damu; hata inakuwa lazima wakinze maagizo ya mahakama ambayo hupingana na imani yao. (Matendo 15:28, 29; 1 Petro 4:3, 4) Na katika siku hizi za kupanda kwa ukosefu wa kazi, inazidi kuwa vigumu kwa Mkristo wa kweli kuepuka kazi ambayo ingemaanisha kuvunja ukamilifu wake mbele za Mungu.—Mika 4:3, 5.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki