Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Shangwe na Matatizo ya Kuwalea Watoto Wanane Ili Wafuate Njia za Yehova
    Mnara wa Mlinzi—2006 | Januari 1
    • Wakati huo, kwa ujumla watu walikubali kwamba uasherati ni kosa. Lakini, mimi na watu wengine wengi tuliamini kwamba waasherati ni wale tu wanaofanya ngono pamoja na watu wengi. Hivyo, tuliamini kwamba si dhambi kwa watu wawili ambao hawajaoana kufanya ngono pamoja maadamu hawafanyi ngono na mtu mwingine. (1 Wakorintho 6:9, 10; Waebrania 13:4) Kwa sababu ya kuwa na maoni hayo, nilipata watoto sita kabla ya kuolewa.

  • Shangwe na Matatizo ya Kuwalea Watoto Wanane Ili Wafuate Njia za Yehova
    Mnara wa Mlinzi—2006 | Januari 1
    • Wakati huo, nilikuwa nikiishi pamoja na baba ya watoto wangu watatu kati ya watoto wangu sita. Hatukuwa tumefunga ndoa. Kupitia Biblia, nilijifunza kwamba Mungu hushutumu ngono nje ya ndoa, na dhamiri yangu ilianza kunisumbua. (Methali 5:15-20; Wagalatia 5:19) Upendo wangu kwa ajili ya ukweli ulipoongezeka, nilitamani kuishi kulingana na sheria ya Mungu. Hatimaye, nikafanya uamuzi. Nilimweleza mwanamume huyo tuliyeishi naye kwamba tusipofunga ndoa basi nitakatiza uhusiano wetu. Ingawa hakukubali mambo niliyoamini, tulifunga ndoa kisheria mnamo Agosti 15, 1970, miaka mitano baada ya Mashahidi kuzungumza pamoja nami kwa mara ya kwanza.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki