Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Watu Wanayaonaje Maadili ya Kiroho Leo?
    Mnara wa Mlinzi—2003 | Aprili 15
    • Idadi ya Wakatoliki nchini Ufaransa ambao huhudhuria Misa kila Jumapili inapungua kwa asilimia 10, na ni asilimia 3 hadi 4 tu ya Wakatoliki wanaoishi Paris ambao huenda kanisani kwa ukawaida.

  • Watu Wanayaonaje Maadili ya Kiroho Leo?
    Mnara wa Mlinzi—2003 | Aprili 15
    • Miaka 100 hivi iliyopita kulikuwa na makasisi 14 kwa watu 10,000 nchini Ufaransa, lakini leo kuna kasisi 1 tu kwa watu 10,000. Barani Ulaya, makasisi wanazidi kuzeeka, na upungufu huo umeathiri nchi ya Ireland na Ubelgiji pia. Vilevile, idadi ya watoto wanaohudhuria madarasa ya katekisimu inapungua, na hiyo inasababisha wasiwasi kuhusu kuendelea kuwapo kwa Kanisa Katoliki.

      Watu wamepoteza imani katika dini. Ni asilimia 6 tu ya Wafaransa wanaoamini kwamba “kweli inaweza kupatikana katika dini moja tu,” ikilinganishwa na asilimia 15 katika mwaka wa 1981 na asilimia 50 katika mwaka wa 1952. Watu wanazidi kupoteza upendezi katika dini. Idadi ya watu wanaosema kwamba wao si wafuasi wa dini yoyote imeongezeka kutoka asilimia 26 mwaka wa 1980 hadi asilimia 42 mwaka wa 2000.—Les valeurs des Français—Évolutions de 1980 à 2000 (Maadili ya Wafaransa Kuanzia Mwaka wa 1980 Hadi 2000).

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki