Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wafa kwa Kupiga Makasia
    Amkeni!—2000 | Desemba 22
    • Wahukumiwa kwa Sababu ya Itikadi Yao

      Mwaka wa 1685, Mfalme Louis wa 14 alifutilia mbali Amri ya Nantes, na Uprotestanti ukapigwa marufuku nchini Ufaransa.a Waprotestanti wapatao 1,500 walihukumiwa kupiga-makasia kwenye manchani kwa sababu walikataa kuwa Wakatoliki au walijaribu kutoroka nchini. Kuwaadhibu “waasi wa kidini” kwa njia hiyo kulikuwa kumejaribiwa mwaka wa 1545, wakati ambapo wafuasi 600 wa Waldensesb walipelekwa kwenye manchani kwa amri ya Mfalme Francis wa Kwanza. Wakati wa Louis wa 14, yule aliyeitwa eti mfalme Mkristo, mnyanyaso ulipamba moto.

      Kwa nini Waprotestanti wakapelekwa kwenye manchani? Ofisa mmoja wa mfalme alitaja sababu: “Waasi wa kidini hawawezi kurejeshwa [kwenye Ukatoliki] kwa njia iwayo yote ila kwa lazima.” Mwanahistoria mmoja aongezea hivi: “Mfalme alitumaini kwamba mara baada ya kuonja ‘maisha ya manchani,’ Waprotestanti wengi waliohukumiwa wangeacha dini ambayo walikuwa wamejidhabihu kwelikweli kwa ajili yake.” Hata hivyo, wengi wao walikataa kukana imani yao ili kuwekwa huru. Kama tokeo, kwa kawaida walipigwa kinyama hadharani kwa sababu ya uchochezi wa makasisi wa jeshi Wakatoliki wa manchani hizo. Baadhi yao walikufa; wengine walibaki na makovu ya mapigo kwa maisha yao yote.

      Licha ya jeuri hiyo ya kikatili, Waprotestanti walishiriki kwa bidii imani yao na wengine. Kama tokeo, watu fulani, kutia ndani angalau kasisi mmoja Mkatoliki, wakawa Waprotestanti. Wale walioonwa kuwa hatari sana, Waprotestanti walioelimika, waliondolewa kutoka kwenye manchani na kutupwa katika magereza yaliyo ardhini ili wafie humo. Lakini hilo halikuwazuia wapiga-makasia Waprotestanti kusaidiana, hata walipanga madarasa ya kuwafunza wenzao kujua kusoma na kuandika.

      Wafungwa walitilia maanani kilichowafanya wanyanyaswe. “Kadiri ninavyoteseka, ndivyo ninavyozidi kupenda kweli inayonifanya niteseke,” akaandika Mprotestanti Pierre Serres. Nchi nyingi zilishtuka kusikia kuhusu mnyanyaso wa kidini nchini Ufaransa. Mwaka wa 1713, Malkia Anne wa Uingereza alifaulu kuomba kuachiliwa huru kwa wafungwa wengi. Jambo la kustaajabisha ni kwamba, Waprotestanti waliokuwa wamepigwa marufuku kuondoka Ufaransa sasa walifukuzwa.

  • Wafa kwa Kupiga Makasia
    Amkeni!—2000 | Desemba 22
    • Wafaransa bado hukumbuka kwa majuto manchani hizo. Wanapokabili tatizo, kwa kawaida Wafaransa husema hivi kwa mshangao: “Quelle galère!” au tafsiri sisisi ya Kiswahili ni, “Ni manchani iliyoje!” Mengi tunayojua kuhusu maisha kwenye manchani hizo yanatokana na masimulizi ya kibinafsi yaliyoandikwa na wapiga-makasia Waprotestanti. Licha ya ubaguzi mbaya sana wa kidini, walifanyiza shirika la pamoja la kutoa msaada na utegemezo. Walihitaji kuwa na uvumilivu na tumaini ili waweze kunusurika, nao hawakuwa tayari kuridhiana.

  • Wafa kwa Kupiga Makasia
    Amkeni!—2000 | Desemba 22
    • [Picha katika ukurasa wa 15]

      Maelezo ya Kifaransa yaliyo juu ya picha yasema hivi: “Njia hakika na za unyofu za kuwarejesha waasi wa kidini kwa imani ya Katoliki.” Picha hiyo ni ya mwaka wa 1686

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki