-
Mahali pa Kubatizia Ushuhuda wa Desturi IliyosahaulikaAmkeni!—2007 | Septemba
-
-
Vidimbwi vingine kama kile kilichoko Mariana, Corsica vilikuwa vimefunikwa kwa paa maridadi. Vidimbwi vyenyewe vilikuwa na umbo la mraba, duara, pembe sita, yai, msalaba, au pembe nane. Upana na kina cha vidimbwi vya ubatizo vya zamani kinaonyesha kuwa vilikusudiwa kwa ajili ya kuwabatiza watu wazima. Vilikuwa vikubwa na vingeweza kutoshea angalau watu wawili. Kwa mfano, huko Lyon, jiji lililo mashariki ya kati ya Ufaransa, kuna kidimbwi chenye upana wa mita 3.25. Vidimbwi vingi vilikuwa na ngazi zilizoshuka majini. Mara nyingi ngazi hizo zilikuwa saba.
Wajenzi walihangaika kuhusu mahali ambapo maji yangepatikana. Majengo mengi ya kubatizia yalijengwa karibu na chemchemi za kiasili au kwenye magofu ya bafu za maji moto, kama ile ya Nice, kusini mwa Ufaransa. Mara nyingi maji yaliingizwa na kutolewa kwenye vidimbwi kupitia mabomba. Katika visa vingine maji ya mvua yalichotwa kwenye kisima kilichokuwa karibu.
Mahali pa Kubatizia pa Mt. Yohana huko Poitiers, magharibi mwa Ufaransa, palipojengwa mnamo 350 W.K. hivi, ni mfano mzuri wa mahali pa kubatizia pa “Wakristo” katika karne ya nne. Ndani ya chumba chenye umbo la mstatili, kilichozungukwa na vyumba vingine, kulikuwa na kidimbwi kikubwa cha pembe nane chenye ngazi tatu. Kina cha kidimbwi hicho ni mita 1.41 na upana wa mita 2.15. Kilikuwa kimeunganishwa na mfereji ulioingiza maji jijini kutoka kwenye chemchemi iliyokuwa karibu.
-
-
Mahali pa Kubatizia Ushuhuda wa Desturi IliyosahaulikaAmkeni!—2007 | Septemba
-
-
[Picha katika ukurasa wa 13]
Mahali pa kubatizia pa Mt. Yohana huko Poitiers, Ufaransa
[Picha katika ukurasa wa 13]
Mahali pa kubatizia pa karne ya tano palipojengwa upya huko Mariana, kwenye Kisiwa cha Corsica
[Hisani]
© J.-B. Héron pour “Le Monde de la Bible”/Restitution: J. Guyon and J.-F. Reynaud, after G. Moracchini-Mazel
-