Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Uhuru wa Kidini—Je, Ni Baraka au Laana?
    Amkeni!—1999 | Januari 8
    • Mjadala kuhusu uhuru wa umma na wa kibinafsi umekaziwa na vyombo vya habari. Madai ya kutia kasumba, kutoza fedha kwa nguvu, kutenda watoto vibaya, na uhalifu mwingi ulio mbaya sana yameelekezwa dhidi ya vikundi fulani vya kidini, mara nyingi bila ithibati yenye msingi. Vyombo vya habari vimesambaza sana habari zinazohusisha vikundi vidogo vidogo vya kidini. Majina yenye kushushia hadhi kama vile “dhehebu” au “farakano” sasa yanatumiwa kila siku. Zikiwa chini ya mkazo wa maoni ya umma, serikali hata zimetokeza orodha za zile zinazoitwa eti madhehebu hatari.

      Ufaransa ni nchi ambayo inajivunia utamaduni wake wa uvumiliano na utengano wa dini na Serikali. Nchi hii inajivunia kuwa bara la “Uhuru, Usawa, Udugu.” Lakini, kulingana na kitabu Freedom of Religion and Belief—A World Report, “kampeni ya elimu shuleni ya kuendelezwa kukataliwa kwa harakati mpya za kidini” imependekezwa katika nchi hiyo. Hata hivyo, watu wengi wanafikiri kwamba hatua hii inatishia uhuru wa kidini. Jinsi gani hivyo?

      Tisho kwa Uhuru wa Kidini

      Uhuru wa kweli wa kidini hupatikana tu wakati vikundi vyote vya kidini vinavyostahi na kutii sheria vinapotendewa na Serikali kwa njia sawa. Uhuru huu hukoma wakati Serikali inapoamua bila msingi wowote ni kikundi kipi kati ya vikundi vya kidini si dini, na hivyo kuinyima mapendeleo ambayo Serikali huzipa dini. Gazeti la Time katika mwaka wa 1997 lilisema hivi: “Wazo muhimu la uhuru wa kidini hupoteza maana serikali inapojitwalia bila haki, haki ya kuidhinisha dini kana kwamba inatoa leseni za kuendesha gari kwa madereva.” Hivi karibuni mahakama moja ya rufani nchini Ufaransa ilitangaza kwamba kufanya hivyo “huongoza kwa kufahamu au bila kufahamu, kwenye utawala wa kiimla.”

      Haki za msingi hutishwa pia kikundi kimoja kinapodhibiti vyombo vya habari. Kwa kusikitisha, mambo yanazidi kuwa hivyo katika nchi nyingi. Kwa kielelezo, katika jitihada za kufasiri kikundi kilicho sawa kidini, mashirika yanayopinga madhehebu yamejiweka yenyewe kuwa mwendesha-mashtaka, hakimu, na baraza la mahakama na kisha yamejaribu kutumia vyombo vya habari kulazimisha umma kukubali maoni yao yenye kupendelea. Hata hivyo, kama vile gazeti la habari la Kifaransa Le Monde lilivyosema, kwa kufanya hivyo, nyakati nyingine mashirika haya yanadhihirisha “ufarakano uleule ambao hudai kuuzuia na kutisha kuanzisha mazingira ya ‘uonevu.’” Hilo gazeti la habari liliuliza hivi: “Je, kushutumiwa kijamii kwa vikundi vidogo vidogo vya kidini . . . hakutishi uhuru wa kimsingi?” Martin Kriele, aliyenukuliwa katika Zeitschrift für Religionspsychologie (Gazeti la Saikolojia ya Dini), alisema: “Msako wa uonevu kwa madhehebu hutokeza hangaiko kubwa zaidi kuliko dini nyingi ziitwazo madhehebu na vikundi vyenye kuvutia hisia. Kwa wazi: Raia wasiokiuka sheria wapaswa kuachwa kwa amani. Dini na itikadi zapaswa kuwa huru na kubaki zikiwa huru, katika Ujerumani pia.” Acheni tufikirie kielelezo kimoja.

  • Uhuru wa Kidini—Je, Ni Baraka au Laana?
    Amkeni!—1999 | Januari 8
    • Kwa kuongezea, gazeti moja la Kifaransa lilisema kwamba makala nyingi zinazoshughulikia mafarakano yanayoshukiwa zilitokana na mashirika yanayopinga mafarakano. Je, jambo hili lasikika kuwa njia bora kabisa ya kupata habari isiyopendelea?

      Mahakama na mashirika ya kimataifa yanayoshughulika na haki za kibinadamu za msingi, kama vile UM, yanasema kwamba “tofauti iliyopo kati ya dini na farakano ni bandia sana kuweza kukubaliwa.” Basi kwa nini wengine wanaendelea kutumia neno lenye kushushia hadhi “farakano”? Huu ni ushuhuda zaidi kwamba uhuru wa kidini unatishwa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki