-
“Mambo Haya Lazima Yatukie”Mnara wa Mlinzi—1999 | Mei 1
-
-
6. Ni jambo gani lililotokea kati ya Waroma na Wayahudi mwaka wa 66 W.K.?
6 Wakati wa msimu wa kiangazi huko Yudea mwaka wa 66 W.K., Wazeloti Wayahudi waliongoza shambulio dhidi ya walinzi Waroma waliokuwa katika ngome iliyokuwa karibu na hekalu jijini Yerusalemu, hatua iliyosababisha jeuri katika sehemu nyingine za nchi. Katika kitabu History of the Jews, Profesa Heinrich Graetz asimulia hivi: “Sesho Galo, aliyekuwa na daraka la kutegemeza heshima ya silaha za Waroma akiwa Liwali wa Siria, . . . hangeweza kuendelea kushuhudia uasi ukienea kumzunguka bila kujitahidi kuukomesha. Aliyakusanya majeshi yake, na watawala jirani wakayatuma majeshi yao kwa hiari.” Jeshi hilo lenye wanajeshi 30,000 lilizingira Yerusalemu. Baada ya kupigana kwa kipindi fulani, Wayahudi walikimbilia upande wa nyuma wa kuta karibu na hekalu. “Kwa siku tano mfululizo, Waroma walizishambulia kuta, lakini kila mara walilazimika kurudi nyuma kwa sababu ya mashambulizi ya silaha ya Wayudea. Ni katika siku ya sita tu ndipo walipofaulu kufukua sehemu ya ukuta wa kaskazini mbele ya Hekalu.”
-
-
“Mambo Haya Lazima Yatukie”Mnara wa Mlinzi—1999 | Mei 1
-
-
9, 10. Siku za shambulio la Waroma ‘zilikatwaje zikawa fupi,’ kukiwa na tokeo gani?
9 Je, siku hizo ‘zilikatwa zikawa fupi’ na watiwa-mafuta waliochaguliwa jijini Yerusalemu wakaokolewa? Profesa Graetz adokeza hivi: “[Sesho Galo] hakuona kuwa yafaa kuendelea na mapigano dhidi ya watu waliokuwa na shauku ya kishujaa na hivyo ajiingize katika kampeni ndefu ya vita wakati wa msimu huo, wakati ambapo mvua za vuli zingeanza . . . nazo zingezuia jeshi lisipate maandalizi. Labda kwa sababu hiyo aliamua kwamba ni jambo la busara kukimbia.” Haidhuru ni jambo gani Sesho Galo alikuwa akifikiria, jeshi la Waroma lilikimbia kutoka jijini, nalo likapata pigo la hasara kubwa kutoka kwa Wayahudi waliokuwa wakilifukuza.
-