Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ‘Hatuwezi Kuacha Kusema Juu ya Yesu’
    Mnara wa Mlinzi—2006 | Septemba 15
    • Wapata Thawabu kwa Kutii

      Angalau mshiriki mmoja wa mahakama hiyo kuu anaguswa moyo na maneno haya, “lazima tumtii Mungu kuwa mtawala kuliko wanadamu.” Gamalieli, mwamuzi anayeheshimiwa sana katika Sanhedrini, anashawishi mahakama isikilize shauri la hekima analotoa katika kikao cha faragha. Akitaja mifano ya kale, Gamalieli anaonyesha kwamba si jambo la hekima kuingilia kazi ya mitume. Anamalizia kwa kusema: “Msijiingize katika mambo ya watu hawa, bali waacheni; . . . ama sivyo, huenda mkaonwa kuwa kwa kweli mnapigana na Mungu.”—Matendo 5:34-39.

      Maneno yenye usawaziko ya Gamalieli yanasadikisha mahakama kuu kuwaachilia mitume. Ingawa wanapigwa viboko, mitume hawatishwi kamwe na tukio hilo.

  • ‘Hatuwezi Kuacha Kusema Juu ya Yesu’
    Mnara wa Mlinzi—2006 | Septemba 15
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 9]

      JE, UMEWAHI KUJIULIZA?

      Luka, mwandikaji wa Biblia, alijuaje maneno ambayo Gamalieli alisema katika kikao cha faragha cha Sanhedrini? Huenda Luka alifunuliwa maneno hayo kupitia roho ya Mungu. Labda Paulo (aliyekuwa mmoja wa wanafunzi wa Gamalieli) alimjulisha Luka kuhusu maneno ya Gamalieli. Au huenda Luka aliwasiliana na mshiriki wa mahakama kuu aliyeunga mkono maoni ya mitume.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki