-
Nuru kwa MataifaUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Inaelekea kwamba Yesu Kristo alikuwa akiufikiria unabii huu alipowahimiza wanafunzi wake kurahisisha maisha yao na kuweka masilahi ya Ufalme kwanza. Alisema hivi: “Ikiwa jicho lako lakufanya ukwazike, litupilie mbali; ni bora zaidi kwako kuingia katika ufalme wa Mungu ukiwa na jicho moja kuliko kutupwa ndani ya Gehena ukiwa na macho mawili, mahali ambapo funza wao hafi na ule moto hauzimwi.”—Marko 9:47, 48; Mathayo 5:29, 30; 6:33.
20 Ni mahali gani hapa panapoitwa Gehena? Karne nyingi zilizopita, msomi Myahudi David Kimhi aliandika hivi: “Hapo ni mahali . . . ambapo pamepakana na Yerusalemu, tena ni mahali pa kuchukiza sana, na watu hutupa humo vitu vichafu na mizoga. Vilevile, humo mlikuwa na moto ulioendelea kuwaka ili kuchoma vitu vichafu na mifupa ya mizoga. Kwa hiyo, hukumu ya waovu huitwa Gehinnom kwa njia ya mfano.” Ikiwa, kama vile msomi huyu Myahudi anavyodokeza, Gehena ilitumiwa kama mahali pa kutupia takataka na mizoga ya wale walioonwa hawastahili kuzikwa, basi moto ungekuwa kitu kinachofaa cha kumaliza takataka hizo. Kisichoteketezwa na moto, kingeliwa na funza. Hiyo inaonyesha vizuri kama nini mwisho kamili utakaowapata adui za Mungu!b
-
-
Nuru kwa MataifaUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
b Kwa kuwa kinachoteketezwa na moto katika Gehena ni mizoga, wala si watu walio hai, mahali hapo hapafananishi mateso ya milele.
-