-
Chembe za Urithi, DNA, na WeweAmkeni!—1999 | Septemba 8
-
-
Katika kiini cha kila chembe, kuna maelfu ya chembe za urithi. Hizo ni sehemu mbalimbali za urithi zinazodhibiti chembe na kwa njia hiyo zinaamua baadhi ya tabia zako. Huenda chembe nyingi za urithi zikaamua aina ya damu yako; nyingine, umbile la nywele zako, rangi ya macho yako, na kadhalika. Kwa hiyo kila chembe hubeba maagizo katika chembe za urithi, maagizo yote yanayohitajiwa ili kujenga, kurekebisha, na kuelekeza utendaji wa mwili wako. (Ona mchoro, ukurasa wa 5.)
-
-
Chembe za Urithi, DNA, na WeweAmkeni!—1999 | Septemba 8
-
-
Maelezo sahihi hayakutolewa hadi mwaka wa 1866 wakati mtawa Mwaustria anayeitwa Gregor Mendel alipochapisha nadharia sahihi ya kwanza juu ya urithi. Kutokana na majaribio aliyofanyia njegere, Mendel aligundua kile alichokiita “elementi za urithi za kipekee” zilizojificha ndani ya chembe za uzazi, naye alisisitiza kwamba ndizo zinazopitisha tabia. Hizi “elementi za urithi za kipekee” sasa huitwa chembe za urithi.
Mnamo 1910, chembe za urithi zilipatikana katika chembe zinazoitwa kromosomu. Kromosomu hasa ni protini na DNA (deoxyribonucleic acid). Kwa kuwa wanasayansi tayari walijua umuhimu wa protini katika utendaji mwingine wa chembe, walifikiri kwa miaka mingi kwamba protini za kromosomu hubeba habari za urithi. Kisha, mnamo 1944, watafiti wakatokeza uthibitisho wa kwanza wa kwamba chembe za urithi hufanyizwa kwa DNA wala si protini.
-