-
Je, Sayansi Itamaliza Magonjwa?Amkeni!—2007 | Januari
-
-
◼ Genomics Taaluma ya muundo wa chembe za urithi inaitwa genomics. Kila chembe katika mwili wa mwanadamu ina vitu vingi sana ambavyo ni muhimu kwa ajili ya uhai. Moja kati ya vitu hivyo ni chembe za urithi. Kila mmoja wetu ana chembe za urithi 35,000 ambazo huamua rangi ya nywele, rangi ya ngozi na macho, kimo, na mambo mengine kuhusu umbo la kila mmoja wetu. Pia chembe zetu za urithi huamua ubora wa viungo vyetu vya ndani.
Chembe za urithi zinapoharibiwa zinaweza kuathiri afya yetu. Kwa kweli, watafiti fulani wanaamini kuwa magonjwa yote husababishwa na kasoro katika chembe za urithi. Sisi hurithi chembe fulani zenye kasoro kutoka kwa wazazi wetu. Chembe nyingine za urithi huharibiwa na vitu vyenye kudhuru katika mazingira.
Wanasayansi wanatumaini kuwa karibuni wataweza kugundua chembe hususa za urithi zinazosababisha tuwe wagonjwa. Hilo litawawezesha madaktari kuelewa kwa nini ni rahisi kwa watu fulani kupata kansa kuliko wengine au kwa nini aina fulani ya kansa ina madhara zaidi kwa watu fulani kuliko wengine. Huenda pia genomics ikafunua kwa nini dawa fulani hufanya kazi inapotumiwa na wagonjwa fulani ilhali inakosa kufanya kazi kwa wengine.
Habari hizo hususa kuhusu chembe za urithi huenda zikatokeza matibabu ya kibinafsi. Unaweza kufaidikaje na teknolojia hiyo? Wazo la matibabu ya kibinafsi linaonyesha kwamba matibabu yatatolewa kuambatana na maelezo kuhusu chembe zako za urithi. Kwa mfano ikiwa uchunguzi wa chembe zako za urithi utaonyesha kwamba una uwezekano wa kupata ugonjwa fulani, madaktari wanaweza kugundua ugonjwa huo muda mrefu sana kabla ya dalili zozote kuonekana. Watetezi wanadai kuwa kabla ugonjwa haujatokea, matibabu yanayofaa, chakula, na kubadili tabia kunaweza hata kuzuia ugonjwa wenyewe.
Pia chembe zako za urithi zitawajulisha madaktari kuhusu uwezekano wa mwili wako kuathiriwa na dawa. Huenda habari hiyo ikawasaidia madaktari kuamua aina inayofaa zaidi ya dawa na kiasi unachohitaji. Gazeti The Boston Globe linaripoti hivi: “Kufikia mwaka wa 2020 huenda [matibabu ya kibinafsi] yakatumiwa kwa kiwango kikubwa kuliko yeyote kati yetu anavyoweza kufikiria leo. Dawa mpya zinazotegemea chembe za urithi zitatokezwa ili kuzuia kisukari, ugonjwa wa moyo, ugonjwa wa Alzheimer, schizophrenia, na magonjwa mengine ambayo hugharimu sana jamii yetu.”
-
-
Je, Sayansi Itamaliza Magonjwa?Amkeni!—2007 | Januari
-
-
Genomics
Kwa kuchunguza muundo wa chembe za urithi katika mwili wa mtu, wanasayansi wanatazamia kwamba wataweza kugundua na kuzuia ugonjwa mapema kabla mtu hajapatwa na ugonjwa wenyewe
[Hisani]
Chromosomes: © Phanie/Photo Researchers, Inc. ▸
-