-
Jitihada ya Kutokeza Jamii KamilifuAmkeni!—2000 | Septemba 22
-
-
Bila shaka, kadiri sayansi ya kurekebisha chembe za urithi inavyokuwa na matokeo, ndivyo madaktari wanavyotarajia kuwa na uwezo zaidi wa kugundua na kurekebisha kasoro za chembe za urithi ambazo husababisha au huelekea kuwaletea wanadamu magonjwa mbalimbali. Pia wanasayansi wanatumaini kwamba hatimaye wataweza kutia chembeuzi zisizo za asili kwenye kiinitete cha mwanadamu ili kukilinda dhidi ya magonjwa kama vile ugonjwa wa kutetemeka, UKIMWI, ugonjwa wa sukari, na kansa ya tezi-kibofu na ya matiti. Hivyo mtoto atazaliwa akiwa na mfumo wa kinga wenye nguvu. Pia wanatarajia kubuni dawa “zitakazoboresha” kiinitete kinachokua, labda kwa kurekebisha chembe za urithi ili kuzidisha uwezo wake wa akili au kuboresha kumbukumbu lake.
Ingawa wanasayansi wenye matumaini makubwa hung’amua kwamba itachukua muda mrefu kabla ya wazazi kuweza kuchagua mtoto wanayemtaka kutoka kwenye orodha, watu wengi huvutiwa sana na taraja la kuzaa mtoto anayewafaa kabisa. Baadhi ya watu hubisha kwamba kutotumia tekinolojia kuondoa kasoro za chembe za urithi ni jambo lisilofaa kabisa. Wao husababu kwamba ikiwa si kosa kumpeleka mtoto wako kwenye shule bora na kwa madaktari bora, mbona usijaribu kupata mtoto bora iwezekanavyo?
Shaka Kuhusu Wakati Ujao
Lakini wengine wana shaka. Kwa mfano, kitabu The Biotech Century chasema: “Kama ugonjwa wa sukari, upungufu wa damu, na kansa zitazuiwa kwa kurekebisha chembe za urithi za watu, mbona wasianze na ‘kasoro’ nyingine ndogo kama: kutoweza kuona mbali, upofu-rangi, kutoweza kusoma vizuri, kunenepa kupita kiasi, na kutumia mkono wa kushoto? Kwa kweli, ni nini kitakachozuia jamii kuamua kwamba rangi fulani ya ngozi ni kasoro?”
-
-
Jitihada ya Kutokeza Jamii KamilifuAmkeni!—2000 | Septemba 22
-
-
Pasipo shaka, yaelekea kwamba tekinolojia hiyo mpya haitapatikana kwa urahisi katika nchi maskini ulimwenguni. Tayari nchi nyingi ulimwenguni hazina utunzi wa msingi kabisa wa afya. Hata katika nchi zilizositawi sana, yamkini ni watu matajiri tu watakaoweza kupata tiba ya chembe za urithi.
-