-
Sisi Sote Ni Familia MojaAmkeni!—2009 | Novemba
-
-
Sayansi Inasema Nini?
Uchunguzi wa chembe za urithi (DNA) umethibitisha uwongo wa kwamba watu wa jamii fulani wana chembe zinazowafanya wawe bora kuliko wengine. Watafiti waliowachunguza watu kutoka mabara tofauti waligundua kwamba tofauti zilizopo katika chembe za urithi za watu waliotoka sehemu yoyote ulimwenguni ilikuwa asilimia 0.5 hivi.a Na asilimia 86 hadi 90 ya tofauti hizo zilipatikana kati ya watu wa rangi ileile. Kwa hiyo, ni asilimia 14 tu ya tofauti hizo inayopatikana kati ya watu wa rangi tofauti.
Kwa kuwa “wanadamu wana muundo unaofanana wa chembe za urithi,” linasema jarida Nature, “elimu hiyo inapaswa kuwa muhimu ili kutatua tatizo la ubaguzi wa rangi.”
-
-
Sisi Sote Ni Familia MojaAmkeni!—2009 | Novemba
-
-
a Hata hivyo, tofauti hizo chache za chembe za urithi ni muhimu sana katika tiba kwa sababu magonjwa fulani huwaathiri watu wa jamii fulani tu.
-