-
Kuchora Ramani za Mbingu Wakati Huo na SasaAmkeni!—2000 | Januari 22
-
-
“Anga la Kikristo Lenye Nyota Nyingi”
Mnamo mwaka wa 1627, msomi Mjerumani Julius Schiller alichapisha kitabu cha ramani za nyota chenye kichwa Coelum Stellatum Christianum (Anga la Kikristo Lenye Nyota Nyingi). Alihisi kwamba wakati ulikuwa umewadia wa kumaliza upagani kwenye mbingu. Hivyo, alianza kuondoa mifano ya kipagani kutoka kwenye anga na akaweka vitu vya Biblia mahali pake. Kitabu The Mapping of the Heavens chaeleza kwamba aligawia “sehemu ya kaskazini mwa mbingu Agano Jipya na ile iliyoko kusini mwake Agano la Kale.” “Kizio cha kusini cha Schiller kiligeuzwa kuwa mfuatano wa habari za Agano la Kale—Yobu achukua mahali pa Mhindi na Tausi, na Kentauro ageuzwa kuwa Abrahamu na Isaka.” Katika Kizio cha Kaskazini, “Cassiopeia awa Maria Magdalen, Perseus awa Mt. Paulo, huku mahali pa ishara kumi na mbili za Nyota za Unajimu pachukuliwa kwa urahisi na wale mitume kumi na wawili.”
Ni kundinyota moja tu lililookoka utakasaji huo. Kundi hilo lilikuwa Columba (Njiwa), linalodhaniwa kuwa linawakilisha njiwa aliyetumwa na Noa kutafuta nchi kavu.
-
-
Kuchora Ramani za Mbingu Wakati Huo na SasaAmkeni!—2000 | Januari 22
-
-
Katikati ya karne ya 19, orodha za vitu zenye mambo mengi zilianza kufanyizwa. Mmojawapo wa watangulizi katika uwanja huu alikuwa mwastronomia Mjerumani Friedrich Wilhelm Argelander. Akishirikiana na wasaidizi kadhaa, alianza mradi mkubwa sana wa kutengeneza orodha ya nyota zilizo kwenye anga la kaskazini. Kwa kutumia darubini-upeo, walipata takriban nyota 325,000 na kupima mahali zilipo na kiasi cha mng’ao wa kila moja. Kwa kuwa mahali pa kuangalia nyota ambapo walifanyia kazi palikuwa katika jiji la Ujerumani la Bonn, orodha hiyo ilikuja kujulikana kuwa Bonner Durchmusterung (Ukaguzi wa Jumla wa Bonn). Ilichapishwa mwaka wa 1863. Baada ya kifo cha Argelander, kazi yake iliendelezwa na mmojawapo wa wasaidizi wake. Alichora ramani ya nyota zilizo sehemu ya kusini mwa anga na kuchapisha kitabu chake kikiwa na kichwa Südliche Bonner Durchmusterung (Ukaguzi wa Jumla wa Kusini mwa Bonn). Ukaguzi wa mwisho ulichapishwa mnamo mwaka wa 1930. Ulitolewa huko Cordoba, Argentina. Orodha hizo zingali na thamani hadi leo hii.
-