Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Marekebisho Yatamaliza Matatizo?
    Amkeni!—2004 | Machi 22
    • Marekebisho Mbalimbali

      Watetezi wa marekebisho wanaweza pia kujaribu kurekebisha mambo ya kawaida. Baadhi yao hutaka kubadilisha kabisa mtindo wa maisha. Mfano mmoja ni harakati ya Lebensreform (marekebisho ya mtindo wa maisha) huko Ujerumani mapema katika karne ya 20. Kwa sababu ya kuongezeka kwa viwanda, watu wengi waliona kwamba maisha hayapendezi na kwamba wanadharauliwa. Wanaharakati walitetea kuishi maisha ya kidesturi. Walitetea mazoezi ya mwili, kufanya shughuli za nje, kutumia dawa za asili, na kutokula nyama.

  • Je, Marekebisho Yatamaliza Matatizo?
    Amkeni!—2004 | Machi 22
    • Marekebisho pia yanaweza kutumiwa kwa makusudi mengine ambayo nyakati nyingine ni yenye kudhuru. Harakati ya Lebensreform huko Ujerumani ilisaidia kuanzisha dhana ya kuboresha jamii ya wanadamu kwa kuteua wazazi ambao wangezaa watoto wenye nguvu zaidi. Watu wenye siasa kali walitumia vibaya ujuzi huo kuunga mkono chama cha Nazi katika jitihada zake za kuwa na jamii bora.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki