Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuomboleza na Kushangilia Mwisho wa Babuloni
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 15. Kanisa Katoliki katika Ujeremani ya Nazi lilikuwaje na hatia ya damu katika visa viwili?

      15 Katika kitabu chake The Catholic Church and Nazi Germany, Guenter Lewy anaandika: “Wakati Mashahidi wa Yehova walipokandamizwa katika Bavaria Aprili 13 [1933] Kanisa hata lilikubali mgawo liliopewa na Wizara ya Elimu na Dini wa kuripoti juu ya washiriki wa farakano hilo walioendelea kuzoea dini hiyo iliyokatazwa.”

  • Kuomboleza na Kushangilia Mwisho wa Babuloni
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • [Sanduku katika ukurasa wa 270]

      Gharama ya Kuridhiana

      Guenter Lewy anaandika katika kitabu chake The Catholic Church and Nazi Germany: “Kama Ukatoliki wa Ujeremani tangu mwanzo ungalishikamana na mwongozo wa kupinga kwa dhati utawala wa Nazi, historia ya ulimwengu ingaliweza kuchukua mwendo tofauti. Hata kama mng’ang’ano huu ungalikosa mwishowe kabisa kumshinda Hitla na kuzuia uhalifu wake mwingi, kwa oni hili ungaliinua sana hadhi ya kiadili ya Kanisa hilo. Gharama ya kibinadamu kwa ukinzani huu ingalikuwa kubwa bila kukanika, lakini dhabihu hizo zingalikuwa zimetolewa kwa ajili ya kusudi kubwa zaidi ya yote. Hitla akiwa haungwi mkono nyumbani, yamkini hangalithubutu kwenda vitani na kihalisi mamilioni ya maisha yangaliokolewa. . . . Wakati Wajeremani wapinga Unazi walipoteswa mpaka kifo katika kambi za mateso za Hitla, wakati weledi wa Polandi walipochinjwa, wakati mamia ya maelfu ya Warusi walipokufa kama tokeo la kutendwa kama Untermenschen [nusu-binadamu] wa Kislavi, na wakati binadamu 6,000,000 walipouawa kimakusudi kwa kuwa ‘si Waarya,’ maofisa wa Kanisa Katoliki katika Ujeremani walitegemeza utawala uliokuwa ukifanya uhalifu huu. Papa katika Roma, kichwa cha kiroho na mwalimu wa kiadili mkuu zaidi ya wote wa Kanisa Katoliki la Roma, alikaa kimya.”—Kurasa 320, 341.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki