Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wamekuwa Marafiki kwa Miaka 60 na Ni Kama Urafiki wao Umeanza Tu
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Oktoba 15
    • Hatimaye Ndugu Erich Frost, mtumishi wa tawi, akaja na kuwasalimu kwa uchangamfu kwa lugha ya Kiingereza. Mambo yalianza kuboreka.

  • Wamekuwa Marafiki kwa Miaka 60 na Ni Kama Urafiki wao Umeanza Tu
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Oktoba 15
    • Ndugu Frost, akiwa mwenye shauku kama kawaida, alianza kusema jambo fulani katika Kijerumani lililoonekana kuwa zito sana. Wengi katika familia walikaa kimya kabisa, huku wakitazama tu sahani zao. Ingawa Wanabetheli hao wapya hawangeweza kuelewa jambo lililokuwa likisemwa, pole kwa pole walianza kutambua kwamba liliwahusu. Kwa hiyo, Ndugu Frost aliposema kwa mshindo, “VERBOTEN!” (“Marufuku!”) na kukazia neno hilo tena na tena kwa sauti kubwa zaidi, ndugu hao waliogopa. Ni nini walichofanya kilichomkasirisha sana?

      Baada ya chakula, watu wote walienda haraka katika vyumba vyao. Baadaye, ndugu mmoja alitueleza hivi: “Ili mweze kutusaidia, ni lazima mjue kuongea Kijerumani. Ndiyo sababu Ndugu Frost alisema kwamba kuzungumza nanyi Kiingereza ni VERBOTEN (marufuku) hadi mtakapojua Kijerumani.”

      Familia ya Betheli ilitii agizo hilo mara moja. Shauri hilo halikuwasaidia tu Wanabetheli hao wapya kujifunza Kijerumani bali pia liliwafundisha kwamba shauri linalotolewa na ndugu mwenye upendo, mara nyingi linatufaidi hata ingawa mwanzoni ni vigumu kulifuata. Shauri la Ndugu Frost lilionyesha kwamba anapendezwa na hali nzuri ya tengenezo la Yehova naye anawapenda ndugu zake.a Si ajabu kwamba ndugu hao wanne walimpenda sana!

  • Wamekuwa Marafiki kwa Miaka 60 na Ni Kama Urafiki wao Umeanza Tu
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Oktoba 15
    • a Simulizi lenye kusisimua la maisha ya Ndugu Frost lilichapishwa katika gazeti la Mnara wa Mlinzi la Kiingereza la Aprili 15, 1961, ukurasa wa 244-249.

  • Wamekuwa Marafiki kwa Miaka 60 na Ni Kama Urafiki wao Umeanza Tu
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Oktoba 15
Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki