Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Urusi
    2008 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Lakini Februari 26, 1990, mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Kidini huko Moscow alikutana na wawakilishi wa Mashahidi wa Yehova. Pia manaibu wawili wa mwenyekiti na washiriki wengine watatu walihudhuria mkutano huo. Mashahidi wa Yehova waliwakilishwa na watu 15: ndugu 11 kutoka Urusi na jamhuri nyingine za Muungano wa Sovieti, Milton Henschel na Theodore Jaracz kutoka Brooklyn, na pia Willi Pohl na Nikita Karlstroem kutoka ofisi ya tawi ya Ujerumani.

  • Urusi
    2008 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Naibu mmoja wa mwenyekiti akasema: “Tunahitaji kujua vizuri zaidi mambo mnayoamini kwani hatuelewi baadhi yake. Kwa mfano, katika kitabu kimoja mnasema Mungu ataisafisha dunia na kuondoa serikali zote. Hatuelewi jambo hilo.” Ndugu Pohl alijibu hivi: “Mashahidi wa Yehova hawashiriki vurugu zozote. Ikiwa kitabu kinasema hivyo, kinarejezea unabii hususa wa Biblia. Mashahidi wa Yehova wanahubiri kuhusu Ufalme wa Mungu na uzima wa milele katika paradiso duniani.”

      Naibu huyo akasema, “Imani hiyo haina ubaya wowote.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki