Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Tumegawanywa na Lugha Lakini Tumeunganishwa na Upendo”
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Julai 1
    • katika majiji matano huko Ujerumani—Dortmund, Frankfurt, Hamburg, Leipzig, na Munich.

  • “Tumegawanywa na Lugha Lakini Tumeunganishwa na Upendo”
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Julai 1
    • Maelfu walijitolea kufanya kazi kabla ya kusanyiko ili mahali pa kusanyiko na mazingira yake pafae kwa ajili ya ibada. (Kumbukumbu la Torati 23:14) Kwa mfano, huko Leipzig, Mashahidi wenyeji walifanya kazi nzuri sana ya kusafisha uwanja, na wakaahidi kufanya kazi hiyo tena baada ya kusanyiko. Kwa sababu hiyo, maofisa wa uwanja huo walifuta sheria fulani katika mkataba wa kukodi uwanja iliyodai kiasi kikubwa cha pesa ili kulipia gharama za kusafisha uwanja.

  • “Tumegawanywa na Lugha Lakini Tumeunganishwa na Upendo”
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Julai 1
    • Wale waliohudhuria kusanyiko la Munich walisema hivi: “Tumegawanywa na lugha lakini tumeunganishwa na upendo.”

  • “Tumegawanywa na Lugha Lakini Tumeunganishwa na Upendo”
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Julai 1
    • Katika maeneo ya mashambani ya Bavaria, wageni hao walisimama mahali penye Majumba ya Ufalme, na wakakaribishwa na Mashahidi wenyeji. Kiongozi wa kikundi kimoja ambaye si Shahidi alivutiwa sana na upendo huo wa kindugu. “Tulipokuwa katika basi tukirudi hotelini,” anaripoti mjumbe mmoja, “kiongozi wetu alisema kwamba sisi ni tofauti sana na vikundi vingine vya watalii. Tulikuwa tumevalia vizuri, na wote walishirikiana na wale waliokuwa wakituelekeza. Hakuna aliyetumia lugha chafu wala hapakuwa na mvurugo. Hakuamini jinsi ambavyo watu wasiofahamiana wangeweza mara moja kuwa marafiki wakubwa.”

  • “Tumegawanywa na Lugha Lakini Tumeunganishwa na Upendo”
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Julai 1
    • Wakati wa makusanyiko ya Kijerumani, hotuba zilitolewa pia katika lugha nyingine 18. Huko Dortmund hotuba zilitolewa katika Kiarabu, Kifarsi, Kihispania, Kireno, na Kirusi; huko Frankfurt zilitolewa katika Kifaransa, Kiingereza, na Kiserbia/Kikroatia; huko Hamburg zilitolewa katika Kidenishi, Kiholanzi, Kiswedi, na Kitamili; huko Leipzig zilitolewa katika Kichina, Kipolishi, na Kituruki; na huko Munich zilitolewa katika Kigiriki, Kiitaliano, na katika Lugha ya Ishara ya Kijerumani.

  • “Tumegawanywa na Lugha Lakini Tumeunganishwa na Upendo”
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Julai 1
    • [Picha katika ukurasa wa 9]

      Wajumbe Wakroatia huko Frankfurt walifurahi kupokea “Tafsiri ya Ulimwengu Mpya” katika lugha yao wenyewe

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki