-
Kutokeza Fasihi za Biblia Ili Zitumiwe Katika HudumaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Katika sehemu nyingine ilikuwa vigumu kuanzisha tena shughuli za uchapaji za Sosaiti baada ya vita ya ulimwengu ya pili. Jengo la kiwanda na la ofisi lililo mali ya Sosaiti katika Magdeburg, Ujerumani, lilikuwa katika eneo lililotawalwa na Wakomunisti. Mashahidi Wajerumani walihamia humo tena, lakini waliweza kufanya kazi kwa muda mfupi tu kabla halijanyakuliwa tena. Ili kujazia uhitaji katika Ujerumani Magharibi, kiwanda cha uchapaji kilitakiwa kianzishwe huko. Majiji yalikuwa yameharibiwa kabisa kwa sababu ya kupigwa mabomu. Hata hivyo, upesi Mashahidi waliweza kutumia kiwanda kidogo cha uchapaji kilichokuwa kimetumiwa na Wanazi, katika Karlsruhe. Kufikia 1948 walikuwa na matbaa-tambarare mbili za kuchapia zikiendeshwa mchana na usiku katika jengo walilopewa katika Wiesbaden. Mwaka uliofuata walipanua jengo la Wiesbaden na wakaongeza hesabu ya matbaa mara nne ili kutimiza mahitaji ya idadi iliyokuwa ikikua haraka sana ya wapiga-mbiu wa Ufalme katika sehemu hiyo ya shamba.
-
-
Kutokeza Fasihi za Biblia Ili Zitumiwe Katika HudumaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
[Picha katika ukurasa wa 591]
Wiesbaden, Ujerumani (1975)
-