-
Kutokeza Fasihi za Biblia Ili Zitumiwe Katika HudumaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Uwezo wa Sosaiti wa kutokeza vitabu vilivyojalidiwa ulikuwa unaongezwa pia. Ujalidi fulani ulikuwa umefanywa katika Uswisi na katika Ujerumani mapema kama katikati ya miaka ya 1920. Kufuatia Vita vya Ulimwengu 2, katika 1948 ndugu katika Finland walianza kujalidi vitabu (mwanzoni, kwa mkono sanasana) ili kushughulikia hasa mahitaji ya nchi hiyo. Miaka miwili baadaye ofisi ya tawi katika Ujerumani ilikuwa ikiendesha kifaa cha kujalidi, na baadaye kikafanya kazi ya ujalidi wa vitabu iliyokuwa ikifanywa katika Uswisi.
-
-
Kutokeza Fasihi za Biblia Ili Zitumiwe Katika HudumaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Viwanda vingine 11 vilikuwa vikitokeza fasihi katika Ulaya, na zote hizo zilikuwa zinasaidia kujazia uhitaji wa fasihi wa nchi nyinginezo. Kati ya hizo, Ufaransa ilikuwa ikitoa fasihi kwa nchi 14, na Ujerumani, ambayo ilichapa katika lugha zaidi ya 40, ilikuwa ikisafirisha ugavi mkubwa kwa nchi 20 na ugavi mdogo zaidi kwenye nchi nyinginezo nyingi.
-