Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wamishonari Wasukuma Mpanuko wa Ulimwenguni Pote
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Mialiko kwa waliotazamiwa kuwa wanafunzi kwa ajili ya darasa la kwanza ilipelekwa Desemba 14, 1942. Ilikuwa ni katikati ya kipupwe wakati wanafunzi 100 waliofanyiza darasa hilo walipojiandikisha kwenye majengo ya shule yaliyoko katika upande wa juu wa jimbo la New York, katika South Lansing. Walikuwa wenye nia, wenye hamu, na kidogo wenye wasiwasi. Ingawa mafunzo ya darasa ndiyo yaliyokuwa hangaiko la mara hiyo, hawangeweza kujizuia kujiuliza ni wapi katika shamba la ulimwengu wangeweza kutumwa baada ya kuhitimu.

      Katika hotuba moja kwa darasa hilo la kwanza katika Februari 1, 1943, siku ya kufungua shule, Ndugu Knorr alisema: “Mnapewa matayarisho zaidi kwa ajili ya kazi inayofanana na ile ya mtume Paulo, Marko, Timotheo, na wengine waliosafiri kwenda sehemu zote za Milki ya Roma wakipiga mbiu ya ujumbe wa Ufalme. Iliwabidi waimarishwe kwa Neno la Mungu. Iliwabidi wawe na ujuzi wa wazi kuhusu makusudi Yake. Katika sehemu nyingi iliwabidi wasimame imara wakiwa peke yao dhidi ya wenye vyeo na wakuu wa ulimwengu huu. Huenda mkapatwa na mambo ayo hayo; na Mungu atakuwa nguvu yenu wakati huo.

      “Kuna sehemu nyingi ambako ushahidi kuhusu Ufalme haujatolewa kwa kadiri kubwa. Watu wanaoishi katika sehemu hizo wamo gizani, wamezuiwa humo na dini. Katika baadhi ya nchi hizo ambako kuna Mashahidi wachache imeonwa kuwa watu wa nia njema huwa tayari kusikiliza na wangejishirikisha na tengenezo la Bwana, ikiwa wangefunzwa ifaavyo. Lazima kuwe na mamia na maelfu zaidi ambao wangeweza kufikiwa ikiwa kungekuwa na wafanyakazi wengi zaidi shambani. Kwa neema ya Bwana, kutakuwa na wengi zaidi.

      “SI kusudi la koleji hii kuwatayarisha kuwa wahudumu walioagizwa rasmi. Nyinyi tayari ni wahudumu na mmekuwa watendaji katika huduma kwa miaka mingi. . . . Mtaala wa mafunzo katika koleji ni kwa kusudi hususa la kuwatayarisha kuwa wahudumu wenye uwezo zaidi katika maeneo ambako mtaenda. . . .

      “Kazi yenu kuu ni ile ya kuhubiri gospeli ya Ufalme nyumba hadi nyumba kama vile Yesu na mitume wake walivyofanya. Mtakapokwisha kupata sikio lenye kusikia, pangeni kufanya ziara ya kurudia, anzeni funzo la nyumbani, na kupanga kampuni [kutaniko] ya watu wote kama hao katika jiji au mji. Si kwamba tu itawapendeza kupanga kampuni, bali ni lazima mwasaidie waelewe Neno, mwaimarishe, mwasemeze pindi kwa pindi, mwasaidie katika mikutano yao ya utumishi na katika mipango yao ya kitengenezo. Watakapokuwa wenye nguvu na waweza kujiendeleza na kuhubiri eneo, mnaweza kuondoka kwenda kwenye jiji jingine ili kupiga mbiu ya Ufalme. Pindi kwa pindi huenda mkahitaji kurudi ili kuwajenga katika imani takatifu zaidi na kuwaimarisha katika mafundisho; kwa hiyo kazi yenu itakuwa ile ya kuchunga ‘kondoo wengine’ wa Bwana, na si kuwaacha. (Yn. 10:16) Kazi yenu halisi ni kuwasaidia watu wa nia njema. Ni lazima mchukue hatua ya kwanza kutimiza mambo, lakini mkitegemea uongozi wa Mungu.”a

      Miezi mitano baadaye washiriki wa darasa hilo la kwanza walikamilisha mazoezi yao maalumu. Wao walipata viza, mipango ya usafiri ikafanywa, na wakaanza kwenda kwenye nchi tisa za Amerika ya Latin. Miezi mitatu baada ya kuhitimu kwao, wamishonari waliozoezwa Gileadi wa kwanza kuondoka Marekani walikuwa njiani kuelekea Kuba.

  • Wamishonari Wasukuma Mpanuko wa Ulimwenguni Pote
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • [Picha katika ukurasa wa 522]

      Wanafunzi wa darasa la kwanza la Shule ya Gileadi

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki