Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ukristo wa Mapema na Miungu ya Roma
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Mei 15
    • Madhehebu yaliyojulikana sana katika karne za mapema W.K., ni kama vile madhehebu ya mungu Serapisi na mungu wa kike Isisi wa Misri, madhehebu ya Atargatisi, mungu wa kike wa samaki wa Wasiria, na madhehebu ya Mithra, mungu wa jua wa Waajemi.

      Kitabu cha Biblia cha Matendo kinaonyesha waziwazi mazingira ya kipagani yaliyowazunguka Wakristo wa mapema. Kwa mfano, liwali Mroma wa Kipro alishirikiana na mwanamume Myahudi aliyekuwa mlozi. (Mdo. 13:6, 7) Huko Listra, watu walifikiria kimakosa kwamba Paulo na Barnaba walikuwa Herme na Zeu, miungu ya Wagiriki. (Mdo. 14:11-13) Paulo alipokuwa huko Filipi, alikutana na kijakazi aliyekuwa akifanya uaguzi. (Mdo. 16:16-18) Mtume Paulo alisema kwamba wakaaji wa Athene ‘walionekana kuwa wenye mwelekeo zaidi wa kuogopa miungu kuliko wengine.’ Katika jiji hilo alikuwa ameona pia madhabahu ambayo ilikuwa imeandikwa “Kwa Mungu Asiyejulikana.” (Mdo. 17:22, 23) Wakaaji wa Efeso waliabudu mungu wa kike, Artemi. (Mdo. 19:1, 23, 24, 34) Kwenye kisiwa cha Malta, watu walisema kwamba Paulo alikuwa mungu kwa sababu hakupatwa na madhara baada ya kuumwa na nyoka. (Mdo. 28:3-6)

  • Ukristo wa Mapema na Miungu ya Roma
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Mei 15
    • Kati ya miungu ya Waroma wenyewe, Sumbula (Jupiter) ndiye aliyekuwa mungu mkuu na walimpa jina Optimus Maximus, yaani, aliye bora kabisa na mkuu zaidi. Ilidhaniwa kwamba alijionyesha kupitia upepo, mvua, radi, na ngurumo. Juno, dada ya Sumbula ambaye pia alikuwa mke wake, alihusianishwa na mwezi. Vilevile ilisemekana kwamba alisimamia mambo yote katika maisha ya wanawake. Binti yake, Minerva, alikuwa mungu wa kike wa kazi za mikono, ujuzi wa kazi mbalimbali, sanaa, na vita.

      Waroma walikuwa na miungu mingi sana. Lares na Penates walikuwa miungu ya familia. Vesta alikuwa mungu wa kike wa jiko la kuotea moto. Janus, aliyekuwa na nyuso mbili, alikuwa mungu wa mwanzo wa kila kitu. Kila kazi ya ufundi ilikuwa na mungu wake. Waroma waliamini pia miungu ya vitu visivyoonekana. Pax alikuwa mungu wa kudumisha amani, Salus mungu wa afya, Pudicitia mungu wa kiasi na usafi wa maadili, Fides mungu wa uaminifu, Virtus mungu wa ujasiri, na Voluptas, mungu wa raha. Walifikiri kwamba kila tendo lililofanywa na Waroma waziwazi na faraghani lilihusiana na mapenzi ya miungu. Kwa hiyo, ili kufanikiwa katika jambo lolote, mungu aliyehusika alipaswa kufurahishwa kupitia sala, dhabihu, na sherehe za kidesturi.

      Njia moja iliyotumiwa kujua mapenzi ya miungu ilikuwa kutafuta ishara za bahati. Njia kuu waliyotumia kutafuta ishara za bahati ni kuchunguza viungo vya ndani vya wanyama waliotolewa dhabihu. Walifikiri kwamba hali ya viungo hivyo ilionyesha ikiwa miungu ilikubali au kukataa tendo fulani.

      Kufikia mwisho wa karne ya pili K.W.K., taifa la Roma lilikuwa limeamua kwamba miungu yao mikuu ilifanana na miungu fulani ya Wagiriki. Sumbula alifanana na Zeu, Juno alifanana na Hera, na kadhalika. Waroma walikuwa pia wamekubali hadithi ambazo zilihusianishwa na miungu ya Wagiriki. Hadithi hizo zilisema mambo mabaya kuhusu miungu hiyo, ambayo ilifanya makosa na ilikuwa na udhaifu kama wa wanadamu. Kwa mfano, ilisemekana kwamba Zeu aliwalala wanawake kinguvu na alifanya ngono na watoto, watu walio hai, na pia wafu. Matendo mapotovu ya miungu hiyo—ambayo mara nyingi yalishangiliwa kwa kelele katika majumba ya maonyesho—yaliwachochea waabudu wa miungu hiyo wafanye matendo mapotovu kabisa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki