Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kushikilia kwa Imara Jina la Yesu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Jiji hilo lilisifika sana kwa sababu ya hekalu lalo la Zeusi, au Jupita. Katika muda wa miaka ya 1800 na kitu wachimbuzi wa mambo ya kale walisafirisha madhabahu ya hekalu hilo kuipeleka Ujeremani, ambako ingali inaweza kutazamwa, pamoja na sanamu na michoro mingi ya miungu ya kipagani, kwenye Pergamon Museum katika Berlin.

  • Kushikilia kwa Imara Jina la Yesu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • “Mimi najua mahali unapokaa, yaani, palipo na kiti cha ufalme cha Shetani.” (Ufunuo 2:13a, NW) Kweli kweli, Wakristo hao walizungukwa na ibada ya kishetani. Kuongezea lile hekalu la Zeusi, palikuwapo patakatifu pa Eskulapiusi, kale kamungu ka maponyo. Pargamamu lilisifika pia kuwa kitovu cha lile dhehebu la ibada ya mfalme wa milki. Neno la Kiebrania linalotafsiriwa “Shetani” linamaanisha “Mkinzani,” na “kiti cha ufalme” chake kinawakilisha utawala wake wa ulimwengu kama unavyoruhusiwa kimungu kwa muhula fulani. (Ayubu 1:6, New World Translation Reference Bible, kielezi cha chini) Wingi wa ibada ya sanamu katika Pargamamu ulionyesha kwamba “kiti cha ufalme” cha Shetani kilikuwa kimeimarishwa sana katika jiji hilo. Ni lazima Shetani awe alihisi hasira jinsi gani kwamba Wakristo huko hawakumwinamia katika ibada ya utukuzo wa taifa!

  • Kushikilia kwa Imara Jina la Yesu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • [Picha katika ukurasa wa 43]

      Vithibitisho hivi vya kuenea kwa ibada ya kipagani vinaonyeshwa katika Pergamon Museum katika Berlin

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki