Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Jiji Lenye Uzuri wa Kung’aa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • “Sasa muundo wa ukuta walo ulikuwa yaspa, na jiji lilikuwa dhahabu safi kama kioo changavu.

  • Jiji Lenye Uzuri wa Kung’aa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Pia, malango kumi na mawili yalikuwa lulu kumi na mbili; kila lango lilikuwa limefanyizwa kwa lulu moja. Na njia pana ya jiji ilikuwa dhahabu safi, kama kioo chenye kuona ndani.”—Ufunuo 21:18-21, NW.

      10. Ni nini kinachomaanishwa na uhakika wa kwamba jiji limejengwa kwa yaspa, dhahabu, na “kila namna ya jiwe la thamani”?

      10 Mjengo wa jiji ni wenye uzuri wa kung’aa kikweli. Badala ya vifaa vya ujenzi vya kidunia, visivyodumu kama udongo-mnamo au jiwe, sisi tunasoma juu ya yaspa, dhahabu iliyosafishwa, na “kila namna ya jiwe la thamani.” Lo! jinsi hivyo vinavyotaswiri vifaa vya ujenzi vya kimbingu! Hakuna kitu kingeweza kuwa na uzuri mno zaidi ya hilo. Sanduku la agano la kale lilikuwa limefunikwa kwa dhahabu safi, na katika Biblia elementi hii mara nyingi huwakilisha vitu ambavyo ni vizuri na vyenye thamani. (Kutoka 25:11; Mithali 25:11; Isaya 60:6, 17) Lakini Yerusalemu Jipya zima, na hata njia pana yalo, vimejengwa kwa “dhahabu safi kama kioo changavu,” kutaswiri uzuri na thamani asilia inayoshinda wazo.

      11. Ni nini kinachohakikisha kwamba wale wanaojumlika kuwa Yerusalemu Jipya watawaka kwa ubora ulio wa juu zaidi sana wa usafi wa kiroho?

      11 Hakuna msafishaji vito binadamu anayeweza kutokeza dhahabu yenye usafi hivyo. Lakini Yehova ndiye Msafishaji Stadi. Yeye huketi “akiwa msafishaji na mtakasaji fedha,” na yeye husafisha washiriki waaminifu mmoja mmoja wa Israeli wa kiroho “kama dhahabu na kama fedha,” akiondoa kutoka kwao taka zote. Watu mmoja mmoja ambao wamesafishwa na kutakaswa kikweli, hao pekee ndio mwishowe watajumlika kuwa Yerusalemu Jipya, na katika njia hii Yehova hujenga jiji kwa vifaa vya ujenzi vilivyo hai ambavyo huwaka kwa ubora wa juu zaidi sana wa usafi wa kiroho.—Malaki 3:3, 4, NW.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki