Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Matetemeko ya Dunia Katika Siku ya Bwana
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • na kila mlima na kila kisiwa viliondolewa mahali pavyo.” (Ufunuo 6:14, NW) Kwa wazi hizi si mbingu halisi au milima na visiwa halisi. Lakini hizo zinafananisha nini?

  • Matetemeko ya Dunia Katika Siku ya Bwana
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 24. (a) Katika unabii wa Biblia, ni wakati gani inaposemwa kwamba milima na visiwa vinatikiswa au kuondolewa uimara? (b) ‘Milima ilitikisikaje’ wakati Ninawi ulipoanguka?

      24 Katika unabii wa Biblia, milima na visiwa vinasemwa kuwa vinatikiswa au kuondolewa uimara wakati wa mabadiliko makubwa ya kisiasa. Mathalani, wakati wa kutabiri hukumu za Yehova dhidi ya Ninawi, nabii Nahumu aliandika: “Milima yenyewe imetikisika kwa ajili ya yeye, na vilima halisi vikajikuta vyenyewe vikiyeyuka. Nayo dunia itapinduliwa kwa sababu ya uso wake.” (Nahumu 1:5, NW) Hakuna maandishi yanayoonyesha kuvunjika kokote kwa milima halisi wakati Ninawi ulipoanguka kikweli katika 632 K.W.K. Lakini serikali kubwa ya ulimwengu ambayo hapo kwanza ilionekana kuwa kama mlima katika imara yayo ilianguka ghafula.—Linga Yeremia 4:24.

      25. Kwenye ule mwisho unaokuja wa huu mfumo wa mambo, “kila mlima na kila kisiwa” vitaondolewaje mahali pavyo?

      25 Kwa hiyo, kimantiki “kila mlima na kila kisiwa” kama inavyorejezewa mwanzoni mwa kufunguliwa kwa kifungo cha sita vingekuwa serikali za kisiasa na matengenezo yanayozitegemea ya ulimwengu huu ambazo zimeonekana kuwa imara sana kwa wengi wa aina ya binadamu. Zitatikiswa zitoke mahali pazo, kwa fadhaa na hofu ya wale ambao hapo kwanza waliziitibari. Kama vile unabii huo uendeleavyo kusimulia, hakutakuwa na shaka lolote kwamba ile siku kubwa ya hasira-kisasi ya Yehova na Mwana wake—lile tetemeko la mwisho kabisa ambalo linaondoa matengenezo yote ya Shetani—imekuja ikiwa na kisasi!

      “Angukeni Juu ya Sisi na Kuficha Sisi”

      26. Binadamu wanaopinga enzi kuu ya Mungu watatendaje katika hofu yao, na ni maneno gani ya hofu kuu watakayotamka?

      26 Maneno ya Yohana yanaendelea: “Na wafalme wa dunia na wenye vyeo vya juu na makamanda wa kivita na matajiri na makamambe na kila mtumwa na kila mtu huru wakajificha wenyewe katika mapango na katika yale matungamo-miamba ya milima. Na wao walifuliza kusema kwa milima na kwa matungamo-miamba: ‘Angukeni juu ya sisi na kuficha sisi kutoka uso wa yule Mmoja aliyeketi juu ya kiti cha ufalme na kutoka hasira-kisasi ya Mwana-Kondoo, kwa sababu siku kubwa ya hasira-kisasi yao imekuja, na ni nani anaweza kusimama?’”—Ufunuo 6:15-17, NW.

      27. Ni vilio gani vilivyotamkwa na Waisraeli wasio waaminifu wa Samaria, na maneno hayo yalitimizwaje?

      27 Wakati Hosea alipokuwa akitamka hukumu ya Yehova juu ya Samaria, jiji kuu la ufalme wa kaskazini wa Israeli, yeye alisema hivi: “Sehemu za juu za Beth-aveni, dhambi ya Israeli, kwa kweli zitatoweshwa kabisa. Miiba na mibigili yenyewe itapanda juu ya madhabahu yao. Na kwa hakika watu watasema kwa milima yenyewe, ‘Funikeni sisi!’ na kwa vilima, ‘Angukeni juu ya sisi!’” (Hosea 10:8, NW) Maneno haya yalitimizwaje? Basi, wakati Samaria lilipoanguka kwa Waashuri wakatili katika 740 K.W.K. hapakuwa na mahali pa Waisraeli kukimbilia. Maneno ya Hosea huonyesha hisia ya utotumaini, hofu tupu, na kuachwa walikohisi watu hao walioshindwa. Wala vilima halisi wala matengenezo ya Samaria yaliyokuwa kama milima hayangeweza kuwapa himaya, hata ingawa yalikuwa yameonekana kuwa ya kudumu sana wakati uliopita.

      28. (a) Ni onyo gani ambalo Yesu aliwapa wanawake wa Yerusalemu? (b) Onyo la Yesu lilitimizwaje?

      28 Hali moja na hiyo, Yesu alipokuwa akipelekwa na askari-jeshi Waroma kwenye kifo, yeye alihutubia wanawake wa Yerusalemu na kusema: “Siku zinakuja ambazo katika hizo watu watasema, ‘Wenye furaha ni wale wanawake walio tasa, na matumbo-uzazi ambayo hayakuzaa na matiti ambayo hayakunyonyesha!’ Ndipo wataanza kusema kwa milima, ‘Angukeni juu ya sisi!’ na kwa vilima, ‘Funikeni sisi!’” (Luka 23:29, 30, NW) Ule uharibifu wa Yerusalemu ulioletwa na Waroma katika 70 W.K. umethibitishwa vizuri kimaandishi, na ni wazi kwamba maneno ya Yesu yana maana inayofanana na ile ya maneno ya Hosea. Wakati ule hapakuwa na mahali pa kujificha kwa Wayahudi ambao walikuwa wamebaki katika Yudea. Kokote walikojaribu kujificha katika Yerusalemu, au hata wakati walipokimbilia ngome ya Masada juu ya mlima, wao hawakuweza kuepuka wonyesho wenye jeuri wa hukumu ya Yehova.

      29. (a) Wakati siku ya Yehova ya hasira-kisasi inapokuja, ni nini kitakachopata wale ambao wamejitoa kuunga mkono huu mfumo wa mambo? (b) Ni unabii gani wa Yesu utakaotimizwa wakati Yehova anapoonyesha hasira-kisasi Yake?

      29 Sasa, kule kufunguliwa kwa kifungo cha sita kumeonyesha kwamba kitu fulani kama hicho kitatukia wakati wa siku inayokuja ya hasira-kisasi ya Yehova. Wakati wa kutikiswa kwa mwisho kabisa kwa huu mfumo wa mambo wa kidunia, wale waliojitoa kuuunga mkono watatafuta sana mahali pa kujificha, lakini hawatapata hata pamoja. Dini bandia, Babuloni Mkubwa, tayari imeshindwa vya kusikitisha sana kuwasaidia. Wala mapango katika milima halisi wala matengenezo ya kisiasa na ya kibiashara yaliyo mfano wa milima hayataandaa usalama wa kifedha au msaada mwingine wa aina yoyote. Hakuna kitu kitakachowakinga wasipatwe na hasira-kisasi ya Yehova. Hofu yao imeelezwa vizuri na Yesu: “Ndipo ishara ya Mwana wa binadamu itaonekana katika mbingu, na ndipo makabila yote ya dunia yatajipigapiga yenyewe kwa ombolezo, na yataona Mwana wa binadamu akija juu ya mawingu ya mbingu akiwa na nguvu na utukufu mkubwa.”—Mathayo 24:30, NW.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki