-
Tauni za Yehova juu ya Jumuiya ya WakristoUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
21. Kunakuwa nini wakati malaika wa pili anapopuliza tarumbeta yake?
21 “Na malaika wa pili akapuliza tarumbeta yake. Na kitu fulani kama mlima mkubwa unaowaka moto kilivurumishwa ndani ya bahari. Na theluthi moja ya bahari ikawa damu;
-
-
Tauni za Yehova juu ya Jumuiya ya WakristoUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
24. Ni nini kinachotolewa picha na lile tungamo lililo kama mlima unaowaka moto lililovurumishwa ndani ya “bahari”?
24 Tungamo moja kubwa lililo kama mlima unaowaka moto lavurumishwa ndani ya “bahari” hii. Katika Biblia, mara nyingi sana milima hufananisha serikali. Mathalani, Ufalme wa Mungu unaonyeshwa kuwa kama mlima. (Danieli 2:35, 44) Babuloni yenye kuharibu ilipata kuwa ‘mlima ulioteketea.’ (Yeremia 51:25, NW) Lakini tungamo la mlima ambalo Yohana anaona lingali likiwaka moto. Kuvurumishwa kwalo ndani ya “bahari” kunawakilisha vizuri jinsi, wakati wa na baada ya vita ya kwanza ya ulimwengu, swali linalohusu serikali lilipata kuwa suala lenye kuwaka moto miongoni mwa aina ya binadamu, hasa katika yale mabara ya Jumuiya ya Wakristo. Katika Italia, Mussolini aliingiza Ufashisti. Ujeremani ilikubali Unazi wa Hitla, hali nchi nyinginezo zilijaribu namna mbalimbali za usoshalisti (ujamaa). Badiliko kubwa lilitukia katika Urusi, ambako pinduzi la Bolsheviki lilitokeza serikali ya kwanza ya Ukomunisti, kukiwa na tokeo la kwamba viongozi wa kidini wa Jumuiya ya Wakristo walipoteza nguvu na uvutano wao katika ile ambayo hapo kwanza ilikuwa mojapo ngome zao kubwa.
25. Serikali iliendeleaje kuwa suala lenye kuwaka baada ya Vita ya Ulimwengu 2?
25 Majaribio ya Ufashisti na Unazi yalizimwa na vita ya pili ya ulimwengu, lakini serikali iliendelea kuwa suala lenye moto, nayo bahari ya kibinadamu iliendelea kusukasuka na kutupa juu serikali mpya za kimapinduzi. Katika ile miongo iliyofuata 1945, hizi ziliwekwa katika mahali kwingi, kama vile China, Vietnamu, Kyuba, na Nikaragua. Katika Ugiriki, jaribio katika serikali ya udikteta wa kijeshi lilishindwa. Katika Kampuchea (Kambodia), jaribio dogo katika Ukomunisti wa ufandamentalisti ulitokeza vifo vinavyoripotiwa kuwa milioni mbili na zaidi.
26. ‘Mlima unaowaka moto’ uliendeleaje kufanyiza mawimbi katika bahari ya aina ya binadamu?
26 Huo ‘mlima unaowaka moto’ uliendelea kufanyiza mawimbi katika bahari ya aina ya binadamu. Ming’ang’ano juu ya serikali imeripotiwa katika Afrika, mabara ya Amerika, Esia, na visiwa vya Pasifiki. Ni jambo linalostahili kuangaliwa kwamba mingi ya ming’ang’ano hii imetukia katika yale mabara ya Jumuiya ya Wakristo au mahali ambako wamisionari wa Jumuiya ya Wakristo wamekuwa wanaharakati wa kisiasa. Mapadri wa Roma Katoliki hata walijiunga na wakapiga vita wakiwa wanachama wa vikosi vya Kikomunisti vya wavamizi wa kupigania Ukomunisti. Wakati uo huo vikundi vya evanjeli ya Kiprotestanti vilifanya kazi katika Amerika ya Kati ili kubadili walichokiita “tamaa mbaya sana na yenye ukatili kwa ajili ya nguvu.” Lakini hakuna yoyote ya misukosuko hii katika “bahari” ya aina ya binadamu imeleta amani na usalama.—Linga Isaya 25:10-12; 1 Wathesalonike 5:3.
27. (a) “Theluthi moja ya bahari” imekuwaje kama damu? (b) ‘Theluthi moja ya viumbe katika bahari’ walikufaje na itakuwaje kwa “theluthi moja ya mashua”?
27 Ule mpigo wa pili wa tarumbeta hufunua kwamba wale wa aina ya binadamu ambao walijihusisha katika mipambano ya kimapinduzi juu ya serikali badala ya kujitiisha kwenye Ufalme wa Mungu ni wenye hatia ya damu.
-