Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kupambana na Hayawani Wawili Wakali Sana
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Mfasili mmoja anaita hayawani-mwitu wa Ufunuo 13:1, 2 “mshenzi,” na kuongeza: “Sisi tunakubali maana zote ambazo θηρίον [the·riʹon, neno la Kigiriki kwa “hayawani”] huwasilisha, kama dubwana mkatili, mharibifu, mwenye kutia kikuli, mlafuaji, n.k.”b Lo! jinsi hiyo inavyoeleza vizuri mfumo wa kisiasa wenye madoa ya damu ambao kwa huo Shetani ametawala aina ya binadamu! Vichwa saba vya huyu hayawani-mwitu husimama kwa ajili ya serikali sita kubwa za ulimwengu ambazo zimeelezwa katika historia ya Biblia kufikia siku ya Yohana—Misri, Ashuru, Babuloni, Umedi-Uajemi, Ugiriki, na Roma—na serikali kubwa ya ulimwengu ya saba iliyotolewa unabii kutokea baadaye.—Linga Ufunuo 17:9, 10.

      6. (a) Vichwa saba vya hayawani-mwitu vilichukua uongozi katika nini? (b) Roma ilitumiwaje na Yehova katika kufikiliza hukumu zake mwenyewe juu ya mfumo wa mambo wa Kiyahudi, na Wakristo katika Yerusalemu walikuwa katika hali gani?

      6 Ni kweli, kumekuwako serikali nyinginezo kubwa za ulimwengu katika historia mbali na zile saba—kama vile hayawani-mwitu ambaye Yohana aliona alivyokuwa na mwili pamoja na vichwa saba na pembe kumi. Lakini vichwa saba huwakilisha zile serikali kubwa ambazo, kila mojapo katika zamu yayo, imechukua uongozi katika kuonea watu wa Mungu. Katika 33 W.K., wakati Roma ilipokuwa mamlaka kuu yenye kutawala, Shetani alitumia hicho kichwa cha hayawani-mwitu kuua Mwana wa Mungu.

  • Kupambana na Hayawani Wawili Wakali Sana
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 9. (a) Ni kwa nini mmoja hapaswi kupinga Biblia inaposema kwamba Shetani humpa hayawani-mwitu mamlaka yake kubwa? (b) Shetani anaelezwaje katika Biblia, naye anatumiaje uvutano juu ya serikali?

      9 Zaidi ya hilo, sababu gani yeyote apinge Biblia inaposema kwamba Shetani ndiye anayewapa hawa hayawani-mwitu mamlaka yao kubwa? Mungu ndiye Chimbuko la taarifa hiyo, na mbele zake ‘mataifa ni kama tone kutoka ndoo na kama filamu tu ya vumbi.’ Mataifa hayo yangefanya vizuri kutafuta kibali cha Mungu kuliko kuudhikia njia ambayo Neno lake hueleza habari zayo. (Isaya 40:15, 17; Zaburi 2:10-12, NW) Shetani si mtu wa hadithi ya uwongo mwenye mgawo wa kuzitesa nafsi zilizoondoka katika moto. Hakuna mahali kama hapo. Badala ya hivyo, Shetani anaelezwa habari zake katika Maandiko kuwa “malaika wa nuru”—stadi wa udanganyi anayetumia uvutano wenye nguvu katika mambo ya kisiasa kwa ujumla.—2 Wakorintho 11:3, 14, 15; Waefeso 6:11-18.

  • Kupambana na Hayawani Wawili Wakali Sana
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Vilevile angalia, drakoni ndiye “akampa hayawani nguvu zake na kiti cha ufalme chake na mamlaka kubwa.” (Linga Luka 4:6.) Hayawani huyo ni ubuni wa Shetani miongoni mwa matungamo ya aina ya binadamu. Kwa kweli Shetani ndiye “mtawala wa ulimwengu huu.”—Yohana 12:31, NW.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki