-
Dhabihu Zilizompendeza MunguMnara wa Mlinzi—2000 | Agosti 15
-
-
13. Fafanua matoleo yaliyotolewa kwa hiari yakiwa zawadi kwa Mungu.
13 Matoleo ya kuchomwa, matoleo ya nafaka, na matoleo ya ushirika ni kati ya matoleo yaliyotolewa kwa hiari yakiwa zawadi au njia ya kumkaribia Mungu ili kupata kibali chake.
-
-
Dhabihu Zilizompendeza MunguMnara wa Mlinzi—2000 | Agosti 15
-
-
14. Toleo la nafaka lilitolewaje?
14 Toleo la nafaka linafafanuliwa kwenye kitabu cha Mambo ya Walawi sura ya 2. Lilikuwa toleo la hiari la unga mwembamba, ambao kwa kawaida ulitiwa mafuta yenye ubani. “[Kuhani] atatwaa konzi moja katika huo unga mwembamba, na katika mafuta yake, na huo ubani wote; kisha kuhani atauteketeza kuwa ndio ukumbusho wake juu ya madhabahu, ni kafara ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza [“kuburudisha,” NW] kwa BWANA.” (Mambo ya Walawi 2:2) Ubani ulikuwa sehemu mojawapo ya uvumba mtakatifu uliochomwa kwenye madhabahu ya uvumba katika tabenakulo na hekalu. (Kutoka 30:34-36) Mfalme Daudi alifikiria hilo aliposema: “Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba, kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni.”—Zaburi 141:2.
-