-
Kwa Nini Ni Muhimu Kuwa na Polisi?Amkeni!—2002 | Julai 8
-
-
Ivan, afisa mmoja wa polisi huko Uingereza, alisema hivi: ‘Ninapenda kuwasaidia watu. Nilivutiwa na kazi hii kwa sababu inahusisha mambo mbalimbali. Kwa kawaida watu hawajui kwamba asilimia 20 hadi asilimia 30 tu ya kazi ya polisi ndiyo inayohusisha kushughulika na uhalifu. Kazi ya polisi inahusisha hasa kuhudumia jamii. Kazi yangu ya kila siku inaweza kuhusisha kushughulikia kifo cha ghafula, msiba wa barabarani, uhalifu, na hata kumsaidia mzee aliyechanganyikiwa. Unaweza kujihisi vizuri sana unapomrudisha mtoto aliyepotea kwa mzazi wake au kumfariji mtu aliyeathiriwa kwa sababu ya uhalifu.’
-
-
Mambo Yaliyotarajiwa na Kuhofiwa Kuhusu PolisiAmkeni!—2002 | Julai 8
-
-
Mambo Yaliyotarajiwa na Kuhofiwa Kuhusu Polisi
MAPEMA katika miaka ya 1800, watu wengi huko Uingereza walipinga mapendekezo ya kuwa na jeshi la polisi lenye mavazi rasmi. Walihofu kwamba polisi wenye silaha ambao wangeongozwa na serikali, wangewanyang’anya uhuru wao. Wengine walihofu kwamba jeshi hilo la polisi lingekuwa kama jeshi la wapelelezi wakali wa Ufaransa ambao walisimamiwa na Joseph Fouché. Hata hivyo, walihitaji sana jeshi la polisi.
Wakati huo London ndilo lililokuwa jiji kubwa na lenye ufanisi mwingi ulimwenguni pote. Uhalifu ulikuwa ukiongezeka na kuhatarisha biashara. Mabawabu waliojitolea kufanya kazi usiku na vilevile majasusi walioitwa Bow Street Runners waliokuwa wakilipwa na watu binafsi hawakuweza kuwalinda watu wala mali zao. Clive Emsley anasema hivi katika kitabu chake The English Police: A Political and Social History: “Watu walizidi kuona kwamba uhalifu na fujo ni mambo ambayo hayapaswi kuwepo katika jamii iliyostaarabika.” Hivyo, wakazi wa London wakaamua kwamba wanataka kuwa na jeshi la polisi, nalo likasimamiwa na Bwana Robert Peel. Mnamo Septemba 1829, polisi wenye mavazi rasmi kutoka katika Kituo cha Polisi cha London wakaanza kufanya doria mitaani.
-