-
Kitabu Kinachotegemeka—Sehemu ya 7Amkeni!—2011 | Mei
-
-
Unabii Unaotegemeka
Serikali ya saba ilianza kujitokeza wakati ambapo Uingereza, ambayo ilikuwa sehemu ya kaskazini-magharibi ya Milki ya Roma, ilipoanza kupata nguvu. Kufikia miaka ya 1760, kisiwa hicho kilikuwa kimeibuka na kuwa Milki ya Uingereza yenye nguvu. Utajiri na nguvu za Uingereza ziliendelea kuongezeka, hivi kwamba katika karne ya 19, ikawa ndiyo nchi tajiri na yenye nguvu zaidi duniani. “Milki ya Uingereza,” kinasema kitabu kimoja, “ilikuwa ndiyo milki kubwa zaidi kuwahi kuonekana ulimwenguni. Ilikuwa na watu milioni 372 na ilienea katika eneo lenye ukubwa wa maili zaidi ya milioni 11 za mraba [kilomita milioni 28 za mraba].”
Hata hivyo, vita vya kwanza vya ulimwengu (1914-1918) vilifanya Uingereza iwe na uhusiano wa pekee na Marekani ambayo hapo awali ilikuwa koloni yake. Matokeo yakawa nini? Mahali pa Milki ya Uingereza pakachukuliwa na muungano wa Uingereza na Marekani, na muungano huo wa nchi mbili zinazotumia Kiingereza na zinazofanana katika njia nyingi ukawa serikali kuu ya ulimwengu ambayo ipo hadi sasa.—Ona sanduku “Muungano wa Pekee.”
-
-
Kitabu Kinachotegemeka—Sehemu ya 7Amkeni!—2011 | Mei
-
-
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 17]
MUUNGANO WA PEKEE
Katika mkutano ambao Rais Barack Obama wa Marekani na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron walifanya pamoja na waandishi wa habari mnamo Julai (Mwezi wa 7) 2010, rais huyo wa Marekani alitangaza hivi: “Lazima tukazie jambo hili. Marekani na Uingereza wana uhusiano wa pekee sana. Tunafurahia urithi uleule. Tuna viwango vilevile. . . . Zaidi ya yote, muungano wetu unafanikiwa kwa sababu tuna malengo yaleyale. . . . Marekani na Uingereza zinapoungana pamoja, watu wetu—na watu wote ulimwenguni—wanakuwa na usalama na ufanisi zaidi. Kwa ufupi, Marekani haina rafiki mwingine wa karibu na mwenye nguvu zaidi kuliko Uingereza.”
-