Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Utawala wa Malkia Elizabeth wa Kwanza—Ulikuwa Wenye Ufanisi?
    Amkeni!—2010 | Januari
    • Mbinu Jasiri ya Philip

      Philip, ambaye wakati huo ndiye aliyekuwa mtawala mwenye nguvu zaidi Ulaya, alijaribu kufanya Uingereza iwe nchi ya Kikatoliki kwa kumposa Elizabeth alipokuwa malkia, lakini Elizabeth akakataa. Kwa miaka mingi, maharamia wa Uingereza walikuwa wakipora meli na bandari za Hispania na kuingilia maeneo ambayo yalikuwa chini ya udhibiti wake wa kikoloni. Pia Philip aliudhika sana Elizabeth alipounga mkono jitihada za Uholanzi za kupigania uhuru dhidi ya utawala wa Hispania. Kuuawa kwa Mary kulimfanya Philip kuchukua hatua. Akichochewa na papa, Philip alipanga kutumia manowari zaidi ya 130 za Hispania. Manowari hizo zingesafiri hadi Uholanzi na kuchukua jeshi kubwa la wanajeshi wa nchi kavu na kisha kuvuka Mlango-Bahari wa Uingereza na kushambulia Uingereza. Kabla ya manowari hizo kukusanywa pamoja, wapelelezi wa Uingereza waligundua njama hiyo. Elizabeth alimtuma Sir Francis Drake akiwa na meli 30 kwenye bandari ya Hispania ya Cádiz, ambapo waliharibu manowari kadhaa za Hispania na hivyo kuchelewesha shambulio la manowari za Hispania kwa mwaka mmoja.

      Hatimaye manowari za Hispania zilipoondoka bandarini mnamo 1588, jeshi la majini la Uingereza lilikuwa tayari. Licha ya kushambuliwa, manowari za Hispania zilifika kwenye Mlango-Bahari wa Uingereza bila kuharibiwa sana na zikatia nanga kwenye bandari ya Calais huko Ufaransa. Usiku uliofuata, Waingereza walituma meli nane zilizojaa mabomu na vitu vinavyoweza kulipuka. Kwa woga, meli za Hispania zilitawanyika, na baada ya mapigano makali, upepo uliovuma kutoka kusini-magharibi ulizisukuma meli hizo kutoka Uingereza hadi Scotland iliyokuwa upande wa kaskazini. Dhoruba huko Scotland na kutoka pwani ya magharibi ya Ireland iliharibu nusu ya meli za Hispania, na zile zilizobaki zilijikokota na kurudi Hispania.

  • Utawala wa Malkia Elizabeth wa Kwanza—Ulikuwa Wenye Ufanisi?
    Amkeni!—2010 | Januari
    • A. Meli zilizojaa mabomu na vitu vinavyoweza kulipuka zilitumwa kushambulia manowari za Hispania

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki