-
Miaka Sabini ya Kushikilia Upindo wa Nguo ya Mtu Aliye MyahudiMnara wa Mlinzi—2012 | Aprili 15
-
-
GILEADI—JAMBO AMBALO SITASAHAU
Mwaka wa 1947, ndugu na dada watano tuliokuwa tukifanya kazi Betheli tulipata mwaliko wa kuhudhuria Shule ya Gileadi huko Marekani, na mwaka uliofuata tulihudhuria darasa la 11. Tulipowasili, kulikuwa na baridi kali sana katika eneo la kaskazini ya New York, mahali ambapo shule hiyo ilikuwa. Jinsi nilivyofurahi kuwa na lile koti ambalo mama yangu alinipatia!
Sitasahau ile miezi sita ambayo niliitumia nikiwa Gileadi. Kuchangamana na wanafunzi wenzangu waliotoka katika nchi tofauti-tofauti 16 kulipanua mtazamo wangu. Zaidi ya manufaa ya kiroho niliyopata kutokana na mambo niliyojifunza Gileadi, nilifaidika na ushirika wa Wakristo wakomavu. Mmoja wa Wakristo hao alikuwa mwanafunzi mwenzangu Lloyd Barry; na pia mmoja wa walimu, Albert Schroeder; na vilevile John Booth, mwangalizi wa Shamba la Ufalme (mahali ambako Shule ya Gileadi ilikuwa) baadaye wote hao walikuja kuwa washiriki wa Baraza Linaloongoza. Ninathamini sana shauri lenye upendo ambalo ndugu hao walinipa na kielelezo chao kizuri cha ushikamanifu kwa Yehova na tengenezo lake.
-
-
Miaka Sabini ya Kushikilia Upindo wa Nguo ya Mtu Aliye MyahudiMnara wa Mlinzi—2012 | Aprili 15
-
-
(Kulia) Nikiwa Shule ya Gileadi mwaka 1948, nimevaa koti la majira ya baridi ambalo Mama alinipa
-