-
Sehemu ya 2—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya DuniaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Katika Mei 1926, George Wright na Edwin Skinner, wakiwa Uingereza, walikubali mwaliko wakasaidie kupanua kazi ya Ufalme katika India. Mgawo wao ulikuwa mkubwa sana! Ulitia ndani sehemu za Afghanistan, Burma (sasa ni Myanmar), Ceylon (sasa ni Sri Lanka), India, na Persia (sasa ni Iran). Walipowasili Bombay, walilakiwa na mvua ya majira. Hata hivyo, kwa kuwa hawakuhangaikia kupita kiasi starehe au raha ya kibinafsi, upesi walikuwa wakisafiri kwenda sehemu za mbali za nchi ili kuwatafuta Wanafunzi wa Biblia waliojulikana ili kuwatia moyo. Pia waliangusha kiasi kikubwa cha fasihi ili kuchochea kupendezwa miongoni mwa wengine.
-
-
Sehemu ya 2—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya DuniaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
[Picha katika ukurasa wa 431]
Alipokwenda India katika 1926, Edwin Skinner alikuwa na mgawo uliotia ndani nchi tano; aliendelea kuhubiri huko kwa uaminifu kwa miaka 64
-