-
Wafalme Washindani Waingia Katika Karne ya 20Sikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
Kuwa washiriki wa mahakama hiyo kulifanya Milki ya Ujerumani na Uingereza zionekane kana kwamba zilipendelea amani. Ziliketi “pamoja mezani,” zikionekana kuwa zenye urafiki, lakini ‘mioyo yao ilinuia kutenda madhara.’ Mbinu ya ‘kusema uwongo walipo pamoja mezani’ haingeweza kuendeleza amani ya kweli. Kuhusu tamaa za kisiasa, kiuchumi, na kijeshi, hakuna chochote ambacho ‘kingefanikiwa’ kwa sababu mwisho wa wafalme hao wawili “utatokea wakati ulioamriwa” na Yehova Mungu.
-
-
Wafalme Washindani Waingia Katika Karne ya 20Sikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
Akitaka kushindana na ukuu wa Uingereza baharini, aliunda jeshi lenye nguvu la majini. “Jeshi la majini la Ujerumani lilianza likiwa duni tu na kukua mpaka likawa la pili baada ya Uingereza katika miaka kumi hivi,” chasema kichapo The New Encyclopædia Britannica. Ili kuudumisha ukuu huo, Uingereza ililazimika kupanua jeshi lake la majini. Uingereza ilifanya maelewano na Ufaransa na maelewano kama hayo pamoja na Urusi, hivyo ikifanyiza Maelewano ya Nchi Tatu. Sasa Ulaya ilikuwa imegawanyika na kuwa kambi mbili za kijeshi— Shirikisho la Nchi Tatu upande mmoja na Maelewano ya Nchi Tatu upande wa pili.
-