-
Utawala wa Malkia Elizabeth wa Kwanza—Ulikuwa Wenye Ufanisi?Amkeni!—2010 | Januari
-
-
Utawala Wenye Ufanisi Waanza
Elizabeth alipoanza kutawala, Uingereza haikuwa ikimiliki maeneo yoyote ng’ambo. Tofauti na hilo, Hispania ilikuwa ikipata mali nyingi kutoka kwa maeneo yake mengi huko Amerika ya Kaskazini, ya Kati, na ya Kusini. Uingereza pia ilitaka kumiliki baadhi ya maeneo hayo. Kwa hiyo, wafanyabiashara wajasiri walisafiri baharini wakitafuta umashuhuri, mali, na njia mpya ambazo zingetumiwa na wafanyabiashara kwenda China na Mashariki ya Mbali. Sir Francis Drake akawa nahodha wa kwanza kuendesha meli yake mwenyewe kuzunguka ulimwengu, akipora meli za Hispania zenye hazina akielekea pwani ya magharibi ya Amerika ya Kusini na Kaskazini. Ili kuzuia udhibiti wa Hispania wa maeneo hayo, Sir Walter Raleigh alianzisha mpango wa kutafuta koloni huko Pwani ya Mashariki ya Amerika Kaskazini. Aliliita eneo alilotwaa, Virginia, kwa heshima ya Malkia Bikira wa Uingereza. Ingawa jitihada za kufanya maeneo ya Amerika ya Kusini na Kaskazini kuwa koloni hazikufanikiwa, zilifanya Uingereza ianze kupendezwa na maeneo hayo. Wakati manowari zenye nguvu za Hispania ziliposhindwa, Uingereza ikawa ndiyo nchi yenye meli nyingi ulimwenguni na Elizabeth aliunga mkono mipango mipya ya kufanya biashara na nchi za kusini-mashariki ya Asia. Msingi ulikuwa umewekwa kwa ajili ya Milki ya Uingereza ambayo ingeenea duniani pote.b
-
-
Utawala wa Malkia Elizabeth wa Kwanza—Ulikuwa Wenye Ufanisi?Amkeni!—2010 | Januari
-
-
Elizabeth alizidi kupata umashuhuri mwishoni mwa karne ya 19 alipotajwa kuwa mwanzilishi wa Milki ya Uingereza, ambayo wakati huo ilikuwa imeenea robo ya dunia.
-
-
Utawala wa Malkia Elizabeth wa Kwanza—Ulikuwa Wenye Ufanisi?Amkeni!—2010 | Januari
-
-
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 22]
JOHN DEE NA MILKI YA UINGEREZA
Elizabeth alimwita John Dee (1527-1608/9) mwanafalsafa wake. John Dee alikuwa mwanahisabati, mwanajiografia, na mwastronomia mwenye kuheshimika, ambaye pia alijihusisha na unajimu na uchawi. Alimshauri malkia kuhusu siku iliyofaa zaidi kutawazwa kwake na alifanya ufundi wake wa kiuchawi katika jumba la malkia. Inasemekana kuwa yeye ndiye aliyetunga usemi “Milki ya Uingereza,” naye alimchochea Elizabeth ajione kuwa malkia wa milki ya wakati ujao ambayo ingeanzishwa kwa kudhibiti bahari na kufanya maeneo mapya kuwa koloni zake. Ili kutimiza hilo, aliwafunza wavumbuzi kuhusu usafiri wa baharini, hasa jinsi ya kutafuta njia ya Kaskazini-Mashariki na Kaskazini-Magharibi kuelekea nchi za Mashariki, na aliunga mkono mipango ya kufanya bara la Amerika Kaskazini kuwa koloni ya Uingereza.
[Hisani]
Photograph taken by courtesy of the British Museum
-