-
Kuimba Wimbo Mpya wa Sherehe ya UshindiUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Huu umati mkubwa utaokoka dhiki kubwa, na waendeleapo kuburudishwa na “vibubujiko vya maji ya uhai,” wao watainuliwa wafikie ukamilifu wa kibinadamu duniani. Wakati fulani baada ya hiyo dhiki kubwa, Hadesi itafanywa kuwa tupu, na mamiloni yasiyohesabika ya binadamu wengine yatafufuliwa na kuwa na fursa ya kunywa kutokana na hayo maji ya uhai. Tukiwa na hilo akilini, ingekuwa sahihi kuuita umati mkubwa matunda ya kwanza ya kondoo wengine—wao ndio wa kwanza ‘kufua majoho yao na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo’ wakiwa na tumaini la kuishi milele duniani.—Ufunuo 7:9, 10, 14, 17; 20:12, 13, NW.
-
-
Kuimba Wimbo Mpya wa Sherehe ya UshindiUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Mwishowe, katika mwezi wa saba wakati vuno lote lilikuwa limekusanywa ndani, kulikuwako Sikukuu ya Vibanda, wakati wa shangwe wa utoaji-shukrani Waisraeli walipokaa kwa juma moja katika vibanda vilivyofanywa kwa, miongoni mwa vitu vingine, matawi ya mitende. (Walawi 23:33-43) Kwa kulingana, umati mkubwa, ambao ni sehemu ya mkusanyo-ndani, hutoa shukrani mbele ya kiti cha ufalme wakiwa na “matawi ya mitende katika mikono yao.”—Ufunuo 7:9, NW.
-