Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mkono wa Yehova Haujawa Mfupi
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • roho yangu iliyo juu yako, na maneno yangu niliyoyatia kinywani mwako, hayataondoka kinywani mwako, wala kinywani mwa wana [“wazao,” “NW”] wako, wala kinywani mwa wajukuu wako, asema BWANA, tangu leo na hata milele.” (Isaya 59:21)

  • Mkono wa Yehova Haujawa Mfupi
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 21. (a) Israeli wa Mungu wametokeza “wazao” gani nyakati za kisasa? (b) “Wazao” hao wanafarijiwaje na agano au mkataba ambao Yehova amefanya pamoja na Israeli wa Mungu?

      21 Leo inaonekana kwamba idadi kamili ya Israeli wa Mungu imekusanywa. Na bado, mataifa yanaendelea kubarikiwa—tena sana. Jinsi gani? Ni kwa vile Israeli wa Mungu wamekuwa na “wazao,” yaani wanafunzi wa Yesu walio na tumaini la kupata uhai wa milele katika dunia-paradiso. (Zaburi 37:11, 29) “Wazao” hao wanafundishwa na Yehova pia na kuagizwa katika njia zake. (Isaya 2:2-4) Ingawa hawabatizwi kwa roho takatifu wala hawaonwi kuwa washiriki katika agano jipya, wanaimarishwa na roho takatifu ya Yehova kushinda vipingamizi vyote ambavyo Shetani huwawekea wanapofanya kazi ya kuhubiri. (Isaya 40:28-31) Sasa idadi yao inafikia mamilioni na inaendelea kuongezeka, huku wakitokeza wazao wao wenyewe. Agano au mkataba ambao Yehova amefanya na watiwa-mafuta huhakikishia “wazao” hao kwamba Yehova ataendelea kuwatumia kuwa wasemaji wake hadi milele.—Ufunuo 21:3, 4, 7.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki