-
“Babuloni Mkubwa Ameanguka!”Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Na mimi nikaona, na, tazama! wingu jeupe, na juu ya wingu mtu fulani ameketi kama mwana wa binadamu, akiwa na taji la dhahabu juu ya kichwa chake na mundu mkali katika mkono wake. Na malaika mwingine [wa nne] akaibuka katika patakatifu pa hekalu, akilia kwa sauti kubwa kwa mmoja anayeketi juu ya wingu: ‘Tia ndani mundu wako na kuvuna, kwa sababu saa imewadia ili kuvuna, kwa kuwa vuno la dunia limeiva kabisa.’ Na yule mmoja anayeketi juu ya lile wingu akatia ndani mundu wake kwenye dunia, na dunia ikavunwa.”—Ufunuo 14:14-16, NW.
-
-
“Babuloni Mkubwa Ameanguka!”Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Lakini ni vuno gani ambalo limetolewa unabii hapa? Alipokuwa duniani, Yesu alifananisha kazi ya kufanya wanafunzi na kuvunwa kwa shamba la ulimwengu wa binadamu. (Mathayo 9:37, 38; Yohana 4:35, 36) Upeo wa kazi hii ya kuvuna unakuja katika siku ya Bwana, wakati Yesu amevikwa taji akiwa Mfalme na anatekeleza hukumu kwa niaba ya Baba yake.
-
-
“Babuloni Mkubwa Ameanguka!”Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Kwanza, kutoka 1919 kuendelea, yeye anaagiza malaika wake wamalize kazi ya kuvuna 144,000. (Mathayo 13:39, 43; Yohana 15:1, 5, 16) Halafu, kazi ya vuno la kukusanya ndani umati mkubwa wa kondoo wengine yatukia. (Yohana 10:16; Ufunuo 7:9) Historia huonyesha kwamba kati ya 1931 na 1935 idadi kubwa kidogo ya hawa kondoo wengine ilianza kutokea. Katika 1935 Yehova alifungulia jamii ya Yohana uelewevu wa utambulisho wa kweli wa huu umati mkubwa wa Ufunuo 7:9-17. Tangu hapo, mkazo mwingi uliwekwa juu ya kukusanya ndani huu umati. Kufikia mwaka 2005, idadi yao ilikuwa imepita alama ya milioni sita, na ingali inaongezeka.
-