-
“Meli za Kitimu” Zatawala BahariniMnara wa Mlinzi—2007 | Oktoba 15
-
-
Meli ya kivita yenye safu tatu za makasia na inayoweza kuelekezwa kwa urahisi, inasafiri kwa mwendo wa kasi zaidi. Wanaume 170 hivi katika safu tatu za makasia wanakaza kabisa misuli yao yenye nguvu wanapopiga makasia, huku wakisogea mbele na nyuma kwenye matandiko ya ngozi yaliyofungiliwa kwenye makalio yao.
Meli hiyo inayosafiri kwa mwendo wa kilomita 13 hadi 17 kwa saa inapita kasi kwenye mawimbi kuelekea meli ya adui. Meli ya adui inajaribu kuepa. Wakati huo hatari, meli hiyo inayumbayumba, nao ubavu wake unaelekeana na meli inayoshambulia. Mdomo wa shaba nyeusi wa meli hiyo ya vita unatoboa ubavu mwembamba wa meli ya adui. Wapiga-makasia wa meli hiyo ya adui wanaogopeshwa na kishindo cha kuvunjika kwa mbao za meli yao na maji ya bahari yanayoingia melini kupitia shimo kubwa lililotobolewa. Kikosi kidogo cha mashujaa wenye silaha nyingi katika meli hiyo ya vita kinapita haraka kwenye ubao wa katikati wa kuingilia melini ili kuwashambulia adui. Ndiyo, meli fulani za kale zilikuwa zenye kutisha kwelikweli!
-
-
“Meli za Kitimu” Zatawala BahariniMnara wa Mlinzi—2007 | Oktoba 15
-
-
[Picha katika ukurasa wa 16]
Umbo la meli ya kivita ya Ugiriki iliyo na safu tatu za makasia
[Hisani]
Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.
-