-
Soko Lililokuwa Kitovu cha Athene la KaleMnara wa Mlinzi—1998 | Julai 15
-
-
Bila shaka, hilo soko lilihitaji mungu-mfadhili wake lenyewe. Mungu huyo alikuwa Zeus Agoraios, aliyedhaniwa kutokeza ufasaha wa kusema. Madhabahu iliyopambwa ambayo ilichongwa kutoka kwa marumaru yenye thamani, ilikuwa imewekwa wakfu kwake. (Linganisha Matendo 14:11, 12.)
-
-
Soko Lililokuwa Kitovu cha Athene la KaleMnara wa Mlinzi—1998 | Julai 15
-
-
Karibu sana na upande wa kaskazini, twaona magofu ya mawe ya chokaa ya hekalu ndogo zaidi, lililojengwa katikati mwa karne ya nne K.W.K. Zeus na Athena Phatrios waliabudiwa hapa, hiyo ilikuwa miungu mikuu ya mashirika mbalimbali ya kidini ya mababa wa kale. Kuwa mshiriki wa mashirika hayo lilikuwa jambo la lazima ili kupewa uraia wa Athene.
-
-
Soko Lililokuwa Kitovu cha Athene la KaleMnara wa Mlinzi—1998 | Julai 15
-
-
Katika Safu ya Nguzo ya Zeus Eleutherios iliyoko karibu, huyo mungu mkuu wa Ugiriki alipewa adhama tena, wakati huu akiwa mungu wa uhuru na ukombozi.
-