-
Matukio Muhimu ya mwaka uliopita2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Konstantinos Kotidis alikuwa mwanajeshi katika jeshi la Muungano wa Sovieti miaka kadhaa kabla ya kuhamia Ugiriki na kuwa mmoja wa Mashahidi wa Yehova. Wenye mamlaka walipotaka Ndugu Kotidis ajiunge na jeshi, hawakumruhusu afanye utumishi wa kiraia badala yake. Walidai kwamba kwa kuwa alikuwa mwanajeshi zamani, hakuwa na msingi wa kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri. Hata hivyo, Baraza la Serikali liliamua kwamba mtu ambaye alikuwa mwanajeshi zamani na ambaye dhamiri yake ilibadilika baadaye kwa sababu za kidini, anaweza kukubaliwa kufanya utumishi wa kiraia badala ya kujiunga na jeshi.
-
-
Matukio Muhimu ya mwaka uliopita2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
[Picha katika ukurasa wa 22]
Konstantinos Kotidis
-